UKUTA (kiferefu chake: Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania) ni jina la kutaja chama kilichoasisiwa na na hayati Mathias Mnyampala mnamo mwaka wa 1965. Lengo kuu la kuanzishwa kwa UKUTA lilikuwa kuendeleza ushairi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla.[1]

Chama kilinuia kusimamia madhumuni kama vile;

  1. Kumasisha matumizi ya Kiswahili fasaha katika jamii
  2. Kutoa mingozo ya utungaji bora wa kazi za fasihi kwa watunzi chipukizi
  3. Kuandaa vitabu vya mashairi ya Kiswahili
  4. Kushirikiana na taasisi nyengine za za ukuzaji wa Kiswahili nchini katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Mathalani kupitia semina na makongamano mbalimbali yanayochochea utumizi mkubwa wa Kiswahili.

UKUTA ilikubwa na changamoto mbalimbali kama zinavyokubwa taasisi nyengine za Kiswahili katika kutimiza majukumu yake ya kukuza na kueneza matumizi ya lugha ya Kiswahili. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazohitaji pesa kuzitatua. Ilikuwa lazima ipatikane fedha ili kuweza kutoa machapisho mbalimbali kwa ajili ya semina na makongamano, upungufu wa watalaamu wa fani ya ushairi na kadhalika. Nyengine ilikuwa kupungua kwa utanzu wa ushauri tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Katika kuhakikisha wanafikia malengo, UKUTA iliweza kufanikiwa kuchapisha baadhi ya mashairi kama vile;

  • (a) Mwaka wa 1997 waliweza kuandika mashairi ya kusifu miaka kumi ya Azimio la Arusha yaliyoitwa Maishairi ya Miaka Kumi ya Azimio la Arusha (UKUTA, 1977) na Ngonjera za UKUTA (1968) kikiwa kama kitabu chao cha kwanza.
  • (b) Kuandaa na kuendesha makongamano kwa waandishi wachanga ili kuwaelimisha kuhusu mbinu za wa mashairi na ngonjera.

MarejeoEdit

  1. "UKUTA | Swahili poets’ association", Encyclopedia Britannica (in English), retrieved 2018-09-02