Ubangi
Mto wa Afrika ya Kati na tawimto la Mto Kongo
(Elekezwa kutoka Ubangi (mto))
Ubangi ni tawimto mkubwa wa mto Kongo na kati ya mito mirefu ya Afrika.
Chanzo | Maungano ya mito Mbomou na Uele mpakani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Mdomo | Mto Kongo (karibu na Mbandaka) |
Nchi | Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo |
Urefu | 850 km, pamoja na Uele 2.272 km |
Tawimito | Mbomou, Uele |
Mkondo | 7,000 m³/s |
Eneo la beseni | 613,202 km² |
Miji mikubwa kando lake | Bangui |
Chanzo chake ni maungano ya mito Mbomou na Uele kwenye mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (J.A.K.) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (J.K.K.).
Mto waelekea kwanza magharibi halafu magharibi-kusini ukipitia mji mkuu Bangui.
Mwendo wote wa mto Ubangi ni mpaka wa kimataifa: kwanza kati ya J.A.K. na J.K.K., halafu kati ya J.K.K. na Jamhuri ya Kongo.
Ubangi waishia katika mto Kongo takriban kilomita 90 kusini kwa mji wa Mbandaka.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Watersheds of Africa: A20 Zambezi Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ubangi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |