Udongo kinamo
Udongo kinamo (pia: udongo wa kinamu, udongo wa mfinyanzi; kwa Kiingereza: clay) ni aina ya udongo ambao una chembechembe ndogo sana na una tabia ya kushikamana.
Udongo wa aina hiyo huwa na uwezo mkubwa wa kushika maji ndani yake. Ganda la udongo kinamo, tofauti na mchanga, haupitiwi na maji kwa urahisi.
Udongo kinamo huwa mgumu ukikauka kabisa. Tangu miaka elfu kadhaa ulitumiwa na binadamu kwa kufinyanga vyombo. Maana udongo huo ukiwa katika hali mbichi unakubali umbo lolote linalopewa na mfinyanzi. Kama unachomwa, yaani kuokwa katika tanuri kwa joto la sentigredi 1000 au zaidi, tabia yake inabadilika. Huwa mgumu, na haubadilishwi tena na maji. Vitu kama matofali ya ujenzi na vyombo kama sahani, vyungu au sufuria hutengenezwa kwa njia hiyo ambavyo vinaweza kudumu miaka mingi visipovunjwa.
Marejeo
hariri
Kujisomea
hariri- S. Guggenheim, R. T. Martin: Definition of Clay and Clay Mineral: Joint Report of the AIPEA Nomenclature and CMS Nomenclature Committees. Ilihifadhiwa 23 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine. (PDF; 168 kB). katika: Clays and Clay Minerals. vol 43, Nr. 2, 1995, uk. 255–256.
- S. Guggenheim, J. M. Adams, D. C. Bain, F. Bergaya, M. F. Brigatti, V. A. Drits, M. L. L. Formoso, E. Galán, T. Kogure, H. Stajnek: Summary of Recommendations of Nomenclature Committees Relevant to Clay Mineralogy: Report of the Association Internationale Pour L’Etudes Des Argiles (AIPEA) Nomenclature Committee for 2006. Ilihifadhiwa 26 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. (PDF; 182 kB). katika: Clays and Clay Minerals. vol 54, Nr. 6, 2006, uk. 761–772.
- S. Hillier: Clay Mineralogy. In: G. V. Middleton, M. J. Church, M. Coniglio, L. A. Hardie, F. J. Longstaffe (ed.): Encyclopedia of sediments and sedimentary rocks. Kluwer Academic Publishers, Dordrecht 2003, uk. 139–142.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Udongo kinamo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |