Ufinyanzi ni teknolojia na ufundi wa kutengeneza vyombo kwa matumizi ya binadamu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi au kauri.

Chungu kinafinyangwa juu ya gurudumu la mfinyanzi
Mfinyanzi akiwa kazini mjini Bangalore, India
Mfinyanzi anatoa chungu kwa kutumia gurudumu
Chombo kilichofinyangwa kwa udongo mjini Hidalgo, Meksico

Udongo wa ufinyanzi unapewa umbo unaotakiwa, kukaushwa, kupambwa na kuchomwa kwa moto na kwa njia hii vyombo vigumu vinatokea kwa matumizi yanayotakiwa kama vile sahani, bakuli, chungu, kikombe au birika.

Udongo unaofaa

hariri

Udongo wa aina ya ufinyanzi ni udongo wa pekee ambao una chembechembe ndogo sana. Chembe zake ni ndogo kuliko mikromita 2. Unapokea maji na kuyashika ndani yake na katika hali ya unyevu ni laini sana una tabia ya kushikamana. Tabia hii inamruhusu mfinyanzi kuupa maumbo mbalimbali.

Lakini baada ya kukauka unakuwa mgumu. Ukichomwa motoni ugumu unaongezeka pia uwezo wake wa kuvumilia kanieneo.

Mbinu za kufinyanga udongo

hariri

Kuna mbinu mbalimbali za kufinyanga vyombo.

  • vipande bapa vya udongo wa mfinyazi vinatandikwa kwa umbo kama chapati, kukatwa na kuunganishwa katika hali bichi halafu kusawazishwa.
  • koili ambazo ni vipande virefu vyembamba vinabingirishwa na kupewa umbo kama kamba halafu kuviringishwa rusu juu ya rusu, halafu uso unasawazishwa.
  • wafinyanzi wengi hutumia gurudumu la mfinyanzi. Kipande cha udongo wa mfinyanzi kinaviringishwa na gurudumu halafu uwazi wa ndani unatengenezwa kwa mkono au kifaa chenye umbo na umbo la nje vilevile.
  • leo hii vyombo vingi vya kufinyangwa vinatengenezwa viwadani wa kutumia mashine na kalibu.

Kukausha vyombo

hariri

Kupamba vyombo

hariri

Kutia kioo

hariri

Kuchoma

hariri

Historia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: