Tofali ni nyenzo inayotumiwa katika ujenzi wa majengo. Kimsingi ni kama jiwe linalotengenezwa na binadamu kutokana na udongo unaofaa hasahasa udongo kinamo.

Ukuta wa matofali yaliyochomwa kwa joto kubwa
Kanisa la Rosklide nchini Denmark ilijengwa kuanzia mwaka 1180 BK kwa kutumia matofali ya kuchomwa

Matofali hutengenenzwa kwa kutumia udongo unaopatikana ambao huchanganywa na maji ili kuweza kushikamanisha udongo huo ili kupokea umbo linalotakiwa.

Udongo unaofaa

hariri

Hivyo tofali hupatikana pale ambapo udongo kinamo unapatikana uliofanywa na punje ndogo za mchanga (kipenyo cha milimita 0,063 hadi 1) pamoja na punje ndogo zaidi za minerali (milimita 0,0002 hadi 0,063) ndani yake lakini isiyo na mata ogania. Udongo kinamo unaweza kushika maji ndani yake na hivyo kuwa na tabia ya plastiki yaani inakubali kubadilishwa maaumbo mbalimbali. Kama udongo kinamo una pande ndogo sana pekee ni udongo wa mfinyanzi lakini kwa matumizi ya matofali si lazima kuwa laini vile. Kama punje ndani yake ni kubwa zaidi tofali haiwezi kuwa imara sana.

Baada ya kukauka tofali imepotea maji ndani yake na kuwa ndogo zaidi; ikipashwa moto punje ndani yake zinashikana na kuwa imara zaidi.

Udongo wote unaweza kuchanganywa na saruji na kuwa imara kwa kukauka tu ilhali ni saruji inaleta uimara kazi ya punje za udongo.

 
Matofali ya udongo wa kukauka huandaliwa katika Romania kwa kuchanganya udongo na manyasi makavu; matofali ni makubwa kwa sababu si imara sana baada ya kukauka
 
Udongo unaandaliwa kwa kuuchanganya na maji
 
Matofali mabichi yanakauka

Uandaaji wa tofali

hariri

Kabla ya kuitwa tofali kitu cha kwanza ni kutafuta mchanga ususani kwa matofali ya simenti lakini kwa matofali ya udongo huwa ni kwanza kutafuta udongo mzuri kwa ajiri ya kushikamanisha na maji baadae. Kwa udongo wa mfinyanzi ni mzuri kuliko udongo mwingine kwa kutengeneza tofali la udongo. Lakini pia kwa matofali ya kuchoma huhitaji udongo mzuri pia unao shikamana kwa ajili ya kutangeneza tofali. Baada ya kutafuta udongo mzuri zoezi la uchanganyaji wa maji huanza kwa aina zote za matofali. Mara nyingi utengenezaji wa matofali huhitaji fremu ya kibao kwa ajili ya kuandaa muundo maalumu wa tofali lenyewe maalumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Katika nchi mbalimbali kuna uzoefu wa kuchanganya udongo na ubua (manyasi makavu) ndani yake; hii inasaidia kushikana tofali kwa ndani na kupunguza uzito.[1]

Aina za matofali

hariri

kuna aina mbalimbali za matofali kutokana na udongo au mchanga unaotumika kutengeneza tofali lenyewe. Aina hizo zinazotokana na udongo au mchanga ni kama zifuatazo

  • Tofali la udongo uliokauka
  • Tofali la kuchoma
  • Tofali la block

Tofali bichi

hariri

Makala kuu:Tofali bichi

Hili ni tofali linalopatikana baada ya kuchanganya udongo mzuri ambao unashikamana vizuri na baada ya hapo udongo huchanganywa na maji ili kuweza kushikamana vizuri na baadae udongo huwekwa kwenye kalibu maalumu ilikutoa tofali husika. Matofali haya yanaweza kudumu kama yanatumiwa katika maeneo penye mvua kidogo. Lakini yakiloweshwa mara nyingi au kwa muda mrefu hupokea maji tena na kupoteza umbo. Inawezekana pia kufunika ukuta wa matofali yaliyokauka kwa lipu. Katika mazingira yabisi sana au jangwani majengo ya matofali mabichi yamedumu karne kadhaa. Tofali bichi ni tofali lenye uwezo mkubwa wa kuhimili majanga.

Tofali la kuchoma

hariri
 
Tanuri ya matofali isiyomalizika; matofali bado ni mabichi

Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutengeneza tofali la udongo na kulichoma kwa kutumia moto. Tanuri ya matofali unafunikwa kwa gana la udongo nje na chini yake moto inawaka kwa siku 2 au 3. Kutengeneza matoli wa njia hii ina gharama zaidi laini matofali yaliyochomwa hudumu zaidi hata penye mvua. Kiasi jinsi udongo mzuiri inapashwa moto zaidi matofali hutoka magumu na bora zaidi.

Tofali la block

hariri

Hili ni tofali linalopatikana baada ya kutumia mchanga pamoja na kuchanganya na simenti tofali hili huwa ni tofali imara kupita matofali yaliyokauka na huweza kujenga nyumba imara sana. Uimara na gharama hutegemea na kiwango cha simenti inayotumiwa. ililiwe tofali

Marejeo

hariri
  1. Linganisha taarifa ya Biblia katika kitabu cha Kutoka 5,6f: Waebrania walipaswa kutafuta manyasi makavu " Farao akawaamuru wasimamizi wa watu.. akisema, 5:7 Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe. "

Viungo vya Nje

hariri