Udongo kinamo

(Elekezwa kutoka Udongo wa mfinyanzi)

Udongo kinamo (pia: udongo wa kinamu, udongo wa mfinyanzi; kwa Kiingereza: clay) ni aina ya udongo ambao una chembechembe ndogo sana na una tabia ya kushikamana.

Udongo wa kinamu nchini Estonia

Udongo wa aina hiyo huwa na uwezo mkubwa wa kushika maji ndani yake. Ganda la udongo kinamo, tofauti na mchanga, haupitiwi na maji kwa urahisi.

Udongo kinamo huwa mgumu ukikauka kabisa. Tangu miaka elfu kadhaa ulitumiwa na binadamu kwa kufinyanga vyombo. Maana udongo huo ukiwa katika hali mbichi unakubali umbo lolote linalopewa na mfinyanzi. Kama unachomwa, yaani kuokwa katika tanuri kwa joto la sentigredi 1000 au zaidi, tabia yake inabadilika. Huwa mgumu, na haubadilishwi tena na maji. Vitu kama matofali ya ujenzi na vyombo kama sahani, vyungu au sufuria hutengenezwa kwa njia hiyo ambavyo vinaweza kudumu miaka mingi visipovunjwa.

Marejeo

hariri


Kujisomea

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Udongo kinamo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.