Yuda (ufalme)

(Elekezwa kutoka Ufalme wa Yuda)

Ufalme wa Yuda (kwa Kiebrania מַמְלֶכֶת יְהוּדָה, Mamlekhet Yehuda) ulikuwa nchi ya Mashariki ya Kati katika karne ya 10 KK hadi karne ya 6 KK.[1][2]Mara nyingi unaitwa ufalme wa Kusini kwa sababu ulitokana na mgawanyiko wa Ufalme wa Israeli ulioendelea upande wa kaskazini.

Ufalme huo uliongozwa daima na ukoo wa Daudi, isipokuwa miaka 6 (842 KK - 837 KK) aliposhikwa utawala malkia Atalia, binti au dada wa mfalme wa Israeli Ahabu. Hata hivyo kwa muda mrefu watawala wa Yuda walikuwa vibaraka wa Ashuru au nchi nyingine za jirani.[3][4]).

Hatimaye, chini ya mfalme Sedekia, mfalme Nebukadneza II wa Babuloni aliangamiza ufalme huo na mji mkuu wake, Yerusalemu, mwaka 587, akihamisha kwa awamu tatu wakazi wake hadi Mesopotamia.

Mwaka 539 Koreshi Mkuu, mfalme wa Persia, aliteka Babuloni na kuruhusu Wayahudi warudi kwao, si tena kama ufalme, bali kama wilaya iliyoitwa Yehud, chini ya Zerubabeli, kitukuu wa Yekonia, wa pili kuanzia mwisho kati ya wafalme wa Yuda.

Tanbihi hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. Grabbe, Lester L., ed. (2008). Israel in Transition: From Late Bronze II to Iron IIa (c. 1250–850 B.C.E.). T&T Clark International. pp. 225–6. ISBN 978-0567027269. 
  2. Lehman in Vaughn, Andrew G.; Killebrew, Ann E., eds. (1992). Jerusalem in Bible and Archaeology: The First Temple Period. Sheffield. p. 149. 
  3. Thompson, Thomas L. (1992). Early History of the Israelite People. Brill. pp. 410–1. 
  4. A History of the Jewish People, H.H. Ben-Sasson ed., Harvard University Press, 1976, page 142: "Sargon's heir, Sennacherib (705-681), could not deal with Hezekiah's revolt until he gained control of Babylon in 702. ..."

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yuda (ufalme) kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.