Ufichamishi

Ufichamishi au kriptografia (kwa Kiingereza: cryptography) ni sayansi ya kulinda mawasiliano kwa kuficha maana yake kwa watu wasiolengwa.

Mashine ya ufichamishi ya Lorenz iliyotumiwa na jeshi la Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili.
Mfumo wa kusogeza herufi kwa nafasi 3
Ufichamishaji kwa fimbo

Kabla ya kupatikana kwa mitambo ya kisasa ujumbe uliandikwa kwa kubadilisha herufi au majina kwa kutumia mfumo uliojulikana kwa mwandishi na mpokeaji aliyelengwa peke yao. Mtu mwingie aliyeona ujumbe alishindwa kuelewa chochote.

Siku hizi ufichamishi hufanywa kwa kutumia mitambo na programu za kompyuta.

Mbinu za ufichamishi sahiliEdit

Kati ya mbinu za ufichamishi zilizotumiwa tangu kale ni kubadilishana herufi kufutana na nafasi zao katika alfabeti. Kwa mfano jemadari wa Roma ya Kale, Julius Caesar, alitunga barua za siri akihamisha kila herufi nafasi tatu. Kwa hiyo nafasi ya "a" ilionyesha badala yake herufi "x", "b" ilionyeshwa kwa "y" na kadhalika.

Mfano salamu ya "habari gani" inasomeka hivi kwa kubadilisha nafasi za herufi

  • kusogeza herufi nafasi tatu: "exyxof dakf"
  • kusogeza herufi nafasi tano: "dwxwne cwje"

Mpokeaji anahitaji tu kujua namba ya ufunguo.

Mbinu nyingine ni ufichamishi kwa fimbo lenye kipenyo fulani unaojulikana tangu Ugiriki ya Kale. Kanda ndefu ya ngozi au papiri iliviringishwa kwenye fimbo. Ujumbe uliandikwa mstari kwa mstari. Kanda ilitolewa na kutumwa kwa mpokeaji. Yule alipaswa kuwa na fimbo lenye unene uleule. Akiviringisha kanda mle aliweza kusoma ujumbe. Mtu mwingine aliona tu herufi bila maana. Kama hakuwa na fimbo lenye unene wa kufaa alishindwa kuona herufi katika mistari jinsi zilivyoandikwa.

MarejeoEdit

  • Kahigi, K. K. (2007). Ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili Sanifu. Kioo cha Lugha, 5(1).

Viungo vya NjeEdit