Ukosoaji wa dini
Ukosoaji wa dini ni mtindo wa kitaalamu wa kuchungulia matamshi ya dini, mafundisho yake na hali yake halisi kwa misingi ya akili ya binadamu bila ya kukubali ukweli wa imani yake, kama matamshi, mawazo na maandiko ya kibinadamu.
Kuna aina na ngazi nyingi za ukosoaji kama vile:
- kuanzia wasiwasi kama mapokeo na desturi ni za kweli au kama watumishi wa dini husika waliongeza au kupunguza ujumbe wake
- kuona wasiwasi kama akili na imani ya kidini zinaweza kwenda pamoja
- kudai uhusiano wa karibu kati ya mahitaji ya jamii, siasa au uchumi na mabadiliko katika dini
- kuona dini ni itikadi ya kibinadamu tu kama mawazo yote mengine
- kukosoa mafundisho ya kale yasiyolingana na wakati lakini yapo katika amri za msingi za dini mbalimbali
na nyingine nyingi.
Ukosoaji wa dini unapatikana kwa namna mbalimbali hata ndani ya jumuiya za kidini, k.mf.:
- mafundisho ya Biblia na ya Korani yanakosoa dini za mataifa za miungu mingi
- Ubuddha ni aina ya dini isiyohitaji dhana ya Mungu
- Uyahudi na Uislamu ni dini ambazo zina wafuasi wasioweza kuamini tena mafundisho ya imani lakini wanajitazama bado kama Waislamu au Wayahudi kwa kuona jumuiya hizo ni za kijamii hata bila ya imani yenyewe. Huwa wanaangaliwa kama wazushi au wasaliti lakini wapo.
- Ukosoaji mkali katika Ulaya ulianzishwa mara nyingi na watu wenye elimu ya Ukristo kama vile Ludwig Feuerbach, Karl Marx na Nietzsche.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |