Chuo Kikuu cha Cape Town

(Elekezwa kutoka University of Cape Town)

Chuo Kikuu cha Cape Town (UCT) ni chuo kikuu cha umma kilicho mjini Cape Town katika jimbo la Rasi ya Magharibi la Afrika Kusini. UCT ilianzishwa mwaka wa 1829 kama South African College, na ndio chuo kikuu kongwe zaidi nchini Afrika Kusini.

Chuo Kikuu cha Cape Town
Staff4,500
Wanafunzi23,500
Wanafunzi wa
shahada ya kwanza
15,800
Wanafunzi wa
uzamili
6,700
Mahali{{{mji}}}
33°57′28″S 18°27′39″E / 33.95778°S 18.46083°E / -33.95778; 18.46083
Former namesSouth African College
RangiDark blue, light blue and white
MsimboIkeys
MascotTiger
AffiliationsAAU, ACU, CHEC, HESA, IAU
Tovutiwww.uct.ac.za
Chuo Kikuu cha Cape Town

Kampasi

hariri
 
Picha ya UCT

Kampasi kuu, inayojulikana kama Upper Campus, iko katika Rhodes Estate kwenye mteremko wa Devil's Peak. Kampasi hii ina, katika eneo lililopakiwa kiasi, na vitivo vya Sayansi, Uhandisi, Biashara, na Masomo ya Kibinadamu (isipokuwa idara za sanaa), vilevile Smuts Hall na makazi ya Fuller Hall. Upper Campus imejengwa kuzunguka Jameson Hall, eneo la mahafali na sherehe nyingine, vilevile mitihani mingi. Majengo ya awali na mpangilio wa Upper Campus uliundwa na JM Solomon na kujengwa kati ya 1928 na 1930. Tangu wakati huo, majengo mengi yameongezwa jinsi chuo kimezidi kukua. Upper Campus pia ni nyumbani kwa maktaba kuu iitwayo Chancelor Oppenheimer Library ambayo ina makala mengi ya Chuo Kikuu, kusanyiko la kama milioni 1.3.

Pamoja na Upper Campus, lakini kutengwa na nyanja za michezo na baraste ya M3, ni kiampasi za Middle na Lower. Kampasi hizi, ambazo zimeenea katika eneo la Rondebosch, Rosebank na Mowbray, zina Kitivo cha Sheria, Chuo cha Afrika Kusini cha Muziki, makazi mengi ya wanafunzi, Ofisi nyingi za usimamizi wa chuo, na vifaa mbalimbali vya michezo. Nyasi bandia ya hali ya juu katika uwanja wa soka imepitishwa na FIFA kutumiwa kwa mafunzo kwa timu za Kombe la Dunia. [1] Kampasi za Upper, Middle na Lower pamoja mara nyingi hujulikana kama "kampasi kuu" au "Rondebosch campus".

Kitivo cha Sayansi ya Afya kiko katika kampasi ya Shule ya Udaktari karibu na Hospitali ya Groote Schuur katika Observatory. Idara za Sanaa bora na Kuigiza ziko kwenye kampasi ya Hiddingh katikati mwa Cape Town. Jengo la kwanza la Chuo hiki, sasa linalojulikana kama Egyptian Building , katika kampasi ya Hiddingh, lilijengwa katika mtindo wa Ufufuo wa Misri. Kampasi nyingine iliyojengwa kwa mtindo huu ilikuwa Medical College of Virginia katika Richmond, Virginia, Marekani. UCT Graduate School of Business Archived 11 Machi 2010 at the Wayback Machine. iko katika kampasi ya Breakwater katika Victoria & Alfred Waterfront.

Muundo

hariri
 
Jameson Hall na Jammie Plaza, mahali spesheli katika kampasi ya juu

Muundo wa Chuo hiki unapatikana katika Katiba ya Chuo Kikuu cha Cape Town, kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya Juu ya 1997 . Kabla ya mwaka wa 2002, ilitolew kwa mujibu wa Sheria ya kibinafsi ya Bunge.

Mkuu wa kielimu wa Chuo Kikuu ni Chansela; hiki ni cheo cha heshima bila nguvu za utendaji. Jukumu la msingi la Chansela ni kutoa shahada kwa niaba ya Chuo, na kukiwakilisha Chuo katika ulimwengu. Chansela wa sasa ni Bi Graça Machel, aliyechaguliwa kwa kipindi cha miaka 10 mnamo Septemba 1999.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Chuo Kikuu ni Makamu wa Chancela (au VC). VC ana wajibu kwa ujumla wa kuunda sera na kutawala Chuo Kikuu. VC wa sasa ni Dkt Max Price, ambaye aliingia mahala pa Profesa Njabulo Ndebele tarehe 1 Julai 2008. VC husaidiwa katika kazi zake na manaibu kadhaa wa Makamu wa Chansela (au DVCs) ambao hushughulikia kazi maalum. Msajili anawajibika kwa taaluma ya utawala wa Chuo Kikuu, vilevile masuala ya kisheria, na ni katibu wa Baraza na Seneti ya Chuo Kikuu.

 
Jengo la Kramer, makao ya Kitivo cha Sheria

Idara za masomo za UCT zimegawanywa katika vitivo sita: Biashara, Uhandisi na Mazingira Yaliyojengwa, Sayansi ya Afya, Masomo ya Kibinadamu, Sheria, na Sayansi; kila kitivo kinaongozwa na Dean. Kituo cha mchanganyiko wa Taaluma kwa Maendeleo ya Elimu ya juu kiko kwenye ngazi sawa na vitivo hivyo. Ingawa Shule ya Uzamili ya Biashara inahesabiwa kuwa sehemu ya Kitivo cha Biashara, huendeshwa na kujitegemea yenyewe na ina Dean wake mwenyewe na Mkurugenzi.

Wanafunzi na wafanyakazi

hariri
 
kumbi za makao za Marquard na Tugwell

Mwaka 2009 23,500 walijiunga na shule, na kati yao 6,700 (asilimia 28.5) walikuwa Wanafunzi Wazamili. Uwiano kati ya wanafunzi wa kike na wa kiume ni karibu 50:50. Zaidi ya asilimia 50 ya mwanafunzi mwili ni wasio wazungu. Wanafunzi wa kimataifa ni takriban asilimia 19 ya jumla katika uandikishaji wa wanafunzi 4300, wakiziwakilisha nchi zaidi ya 100.

UCT huajiri takriban wafanyakazi 4500 ambao asilimia 44 ni wa kitaaluma , wengine kiutawala na wafanyakazi wasaidizi. Mwaka wa 2007 UCT ilikuwa na wafanyakazi kitaaluma wa kudumu 866. Kati ya asilimia 85 na 90 ya wafanyakazi wa kitaaluma wana shahada za PhD au shahada za kwanza. Uwiano wa wafanyakazi wa kitaaluma wasio wazungu kwa sasa ni kama asilimia 23.

Michezo, vilabu, na mila

hariri

UCT ina vilabu 36 vya michezo mbalimbali, pamoja na michezo ya timu, michezo ya kibinafsi, michezo iliyokithiri na michezo ya karate. [2]Timu za michezo za chuo, na hasa timu ya raga, zinayojulikana kama "IKEY Tigers" au "Ikeys". Jina la msimbo la "IKEY" lina asili yake katika miaka ya 1910 kama kama tamko la kejeli ya kiyahudi lililotumiwa kwa wanafunzi wa UCT na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stellenbosch, kwa sababu ya idadi kubwa, ikidhaniwa, ya wanafunzi wa Kiyahudi wa UCT[3]. Stellenbosch ni wapinzani wa jadi wa UCT katika mchezo wa raga; mechi ya kila mwaka kati ya vyuo hivi wiwili huchezwa.

Kuna zaidi ya Vilabu 80 vya mwanafunzi chuoni UCT; hizi zaweza kwa ujumla kuwa katika vitengo tano:[4]

  • jamii za Kisiasa , ikiwa ni pamoja na matawi ya taifa ya vijana ya vyama vya kisiasa.
  • Jamii za kimasomo kwa wale wanaopenda katika taaluma fulani ya kusoma au kusoma mada fulani.
  • Jamii za kidini, ambazo baadhi hujihusisha na madhehebu ya dini au maeneo ya karibu ya kuabudu.
  • Jamii za Kitaifa/kitamaduni kwa wanafunzi kutoka nchi fulani au kabila fulani.
  • Jamii za Maslahi maalum kwa wale wanaopenda shughuli mbalimbali au masuala mbalimbali.

Historia

hariri

Mizizi ya UCT iko katika uanzishwaji wa Chuo cha Afrika Kusini, shule ya wavulana, mnamo 1829. Mwaka wa 1874 sehemu ya elimu ya juu ikajitenga na kuwa Chuo Kikuu na ile ya wanafunzi wachanga ikawa Shule za Kitaaluma za Afrika Kusini.

UCT ilihamia kampasi ya Groote Schuur Estate mwaka wa 1928. Wakati wa mfumo wa kibaguzi, miaka ya 1960-1990, UCT iliendelea kupinga ubaguzi wa rangi, na ilikuwa kiongozi katika ukombozi na uwiano wa kirangi. Mwaka wa 1987 hasa ulikuwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya wanafunzi walioandamana na polisi, na taarifa za polisi kuwepo katika kampasi kudhibitiwa na serikali. Tarehe 24 Aprili 1987 polisi waliingia kampasi na hii ilikuwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1972 kwa huduma ya polisi ya Afrika Kusini kuwahi kusitisha maandamano katika chuo kikuu cha wazungu[5]. Mara nyingi, waandishi wa habari na wahariri wa gazeti rasmi la wanafunzi, Varsity, walijipata chini ya upekuzi kutoka kwa serikali ya kibaguzi ya chama tawala cha National Party.

Nembo ya UCT iliundwa mwaka wa 1859 na Charles Davidson Bell, Soroveya-Mkuu wa Cape Colony wakati huo. Bell alikuwa msanii shupavu ambaye pia aliunda medali na stempu ya pembe tatu ya Cape.

Daraja

hariri

Chuo Kikuu cha Cape Town kinaorodheshwa kama chuo kikuu bora zaidi Afrika yote na THES - QS World University Rankings na Academic Ranking of World Universities na Chuo Kikuu cha Shanghai Jiao Tong. Ndio chuo kikuu pekee Afrika kilichoingia ndani ya 200 bora kulinagana na orodha ya THES-QS ikiwa ya 146, mbele ya vyuo vikuu mbalimbali mashuhuri kama vile Chuo Kikuu cha Tufts na Chuo Kikuu cha London, Malkia Mary. [6] [7]

Mahusiano

hariri

UCT ni mwanachama wa Worldwide Universities Network, Association of African Universities, Chama cha Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Madola, Cape Higher Education Consortium, Elimu ya Afrika Kusini, na Shirikisho la Kimataifa la Vyuo Vikuu.

Wanafunzi wa Zamani Mashuhuri

hariri

Watano wa wahitimu wa Chuo hiki wametuzwa Tuzo ya Nobel:

Wafanyakazi mashuhuri

hariri
  • Mwanakosmolojia George Ellis, anayefanya kazi na Stephen Hawking na mshindi wa 2004 wa Templeton Prize, Profesa anayeheshimika wa Mitambo Migumu katika Idara ya Hisabati na Hesabu tenzi.
  • Mwandishi Andre Brink profesa katika lugha ya Kiingereza na Idara ya Fasihi.
  • Mwandishi Breyten Breytenbach profesa wa kutembelea katika Graduate School of Humanities kuanzia Januari 2000.
  • Profesa David HM Brooks (1950-1996), mwandishi wa 'On living in an Unjust Society', na 'The Unity of the Mind'.
  • Helen Zille, meya wa zamani wa Cape Town na kwa sasa Waziri wa Western Cape, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Umma wa chuo kikuu.
  • UCT ina wafanyakazi wanasayansi wa daraja la A 27 (lilipimwa na National Research Foundation), kumaanisha kuwa wao ni viongozi duniani katika taaluma zao za utafiti.

Utafiti wa kusifika

hariri

Marejeo

hariri
  1. http://www.uct.ac.za/dailynews/?id=7052
  2. "Current Sports Clubs at UCT". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-04-09. Iliwekwa mnamo 2007-06-08. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  3. Swanson, Felicity (2007). "'Die SACS kom terug': intervarsity rugby, masculinity and white identity at the University of Cape Town, 1960s-1970s". Katika Field, Sean; na wenz. (whr.). Imagining the City: Memories and Cultures in Cape Town. Cape Town: HSRC Press. uk. 210. ISBN 0-7969-2179-2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-04-26. Iliwekwa mnamo 2007-06-08. {{cite book}}: Explicit use of et al. in: |editor= (help); External link in |chapterurl= (help); Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20070426132201/http://www.hsrcpress.ac.za/full_title_info.asp?id= ignored (help)
  4. "Student Affairs: Societies". University of Cape Town. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-03. Iliwekwa mnamo 2007-06-08.
  5. [10] ^ Cape Times, ripota mfanyikazi, ukurasa wa mbele, Jumamosi, 25 Aprili 1987. "Sehemu kubwa za Chuo Kikuu cha Cape Town zilikuwa hazikaliki wakati mwingine hapo jana alasiri na baadhi ya mihadhara kukatizwa kwa sababu ya vitendo kwa watu fulani ambayo hayawezi kuripotiwa kwa sababu ni chini ya hali ya dharura serikalini na udhibiti kwa waandishi wa habari. South African Breweries ilipata hasara ya R120,000 wakati moja ya magari yao lilipoteketezwa katika kampasi yake na wanafunzi waliokuwa wakifanya maandamano ya kupinga vifo vya wafanyakazi sita wa reli na kuachishwa kazi kwa 16,000 wengine. Kituo cha serikali cha kutoa habari kutoka idara tofauti, usiku wa jana kililikataza gazeti la Cape Times kuchapisha ukweli kamili wa matukio ya siku huko UCT. Pia walilikataza gazeti hili kuchapisha picha tatu zilizochukuliwa wakati wa mchana, ikiwa ni pamoja na moja ya kuteketezwa kwa gari hilo. Makabiliano ya masaa manne kati ya watu wasiotambulikana na karibu wanafunzi 150-200 yalifuatia mkutano wakati wa chakula cha mchana ulihudhuriwa na wanafunzi 700, ulioitwa kupinga vifo hivyo na kufutwa kazi kwa Wafanyakazi wa Wafanyakazi Reli ya SA na Wafanyakazi wa Umoja wa Bandari (SARHWU) siku ya Jumatano. "
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-20. Iliwekwa mnamo 2010-02-04.
  7. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-01. Iliwekwa mnamo 2010-02-04.

Viungo vya nje

hariri