Shemasi (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kigiriki: διάκονος, diákonos[1] maana yake "mtumishi", "msaidizi", "mhudumu", au "mjumbe".[2]) ni kiongozi wa Kanisa anayeunganisha wenye daraja za juu na walei.

Shemasi wa Kanisa Katoliki huko Polandi akiimba mbiu Exsultet usiku wa Pasaka.
Shemasi wa Kiorthodoksi katika mavazi yake rasmi.

Hii ni kwa sababu ushemasi ni daraja ya tatu na ya mwisho katika Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa ya Ukristo. Unatolewa na Askofu kwa kumwekea muumini mikono na kumuombea ili atoe vizuri huduma ya Neno la Mungu, ya liturujia na ya matendo ya upendo. Unaweza kutolewa kwa namna ya kudumu au kama hatua ya kuelekea daraja ya upadri.

Katika Kanisa la Moravian ushemasi ni ngazi ya kwanza ya uchungaji.

Katika historia ya Kanisa mashemasi waliotoa mchango mkubwa, mara nyingi kwa kukamilisha ushuhuda wao kwa kumfia Yesu.

Kati yao maarufu zaidi ni Laurenti Mfiadini, Efrem wa Syria, na Fransisko wa Asizi.

Katika Biblia hariri

Imezoeleka kusema ushemasi ulianzishwa na Mitume walipoweka viongozi saba wenye kusema Kigiriki kuwasaidia katika kuongoza Kanisa la Yerusalemu[3][4]. Wa kwanza wao alikuwa Stefano [5]. Hata hivyo wataalamu wengine wanasema hao saba hawakuwa mashemasi tu.

Kwa vyovyote cheo cha ushemasi kinazungumziwa na Agano Jipya, hasa katika Nyaraka za Kichungaji, Mtume Paulo anapotaja sifa za shemasi (1Tim 3:1-13).

Tanbihi hariri

  1. deacon. The American Heritage Dictionary of the English Language. Bartleby (2000). Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-01-25. Iliwekwa mnamo 2008-08-17.
  2. Liddell, Henry George; Scott, Robert (1889). An Intermediate Greek-English Lexicon. Oxford: Clarendon Press. ISBN 0-19-910206-6. Retrieved 2007-10-18. 
  3. Thurston, Herbert (1913). "Deacons". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. http://www.newadvent.org/cathen/04647c.htm. Retrieved 2007-10-18.
  4. Hopko, Thomas. Holy Orders. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-10-21. Iliwekwa mnamo 2007-10-18.
  5. Mdo 6

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shemasi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.