Utakaso wa kikabila

Utakaso wa kikabila ni maneno ambayo yamekuja kutumika kwa upana kuashiria aina zote za fujo zinazohusisha ukabila, kuanzia mauaji, ubakaji na mateso na hata kuhamisha wakazi kwa lazima. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1993 ilifafanua utakaso wa kikabila kwa ufasaha kama, "kupangwa kimaksudi kuwatoa kutoka eneo fulani, watu wa kabila fulani, kwa kutumia nguvu au kwa kuwaogofya, ili kufanya eneo hilo liwe na kabila moja tu."


Neno utakaso wa kikabila ni tofauti na neno mauaji ya kimbari. Maneno haya hayalengi maana sawa, hata hivyo utafiti wa kisomi unaonyesha kuwa maneno haya yote yanaweza kutumiwa kuelezea aina nyingi za ushambulizi dhidi ya mataifa au makabila yenye msingi wa kidini. Kwa ufupi, utakaso wa kikabila ni sawa na kuhamisha watu kutoka nchi fulani kwa lazima huku mauaji ya kimbari yakiwa sawa na "mauaji ya kimakusudi ya kundi fulani la kikabila, kidini au kitaifa kwa sehemu au kwa ujumla."

Dhana katika utakaso wa kikabila ni "kuwalazimisha watu kuhama, na mbinu zinazotumiwa kufanya hivi huenda zikawa za kisheria au zenye nguvu chache za kisheria." Kwa hivyo, dhana hizi mbili ni tofauti, lakini hata hivyo zina uhusiano,"kwa maana ya kawaida na maana ya ndani, utakaso wa kikabila unasababisha mauaji ya kimbari, kwa njia ya mauaji ya halaiki ya watu yanayotendwa ili kufanya watu fulani wahame kutoka eneo fulani."

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utakaso wa kikabila kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.