Utengule
ukarasa wa maana wa Wikimedia
Utengule ni jina la sehemu tofauti kusini mwa Tanzania:
- Utengule Usongwe katika wilaya ya Mbeya Vijijini takriban 17 km kutoka Mbeya upande wa kusini-magharibi.
- Utengule Usangu katika wilaya ya Mbarali.
Utengule hizo mbili zina uhusiano wa kihistoria kama makao makuu ya chifu Merere II wa Wasangu aliyehamisha boma lake mwaka 1877 kutoka Usangu kwenda Usafwa kutokana na mashambulio ya Wahehe na kuita boma jipya tena "Utengule".
Kuna pia kata za:
- Utengule (Mlimba) katika Wilaya ya Mlimba, Mkoa wa Morogoro
- Utengule (Makambako) katika wilaya ya Makambako Mjini, Mkoa wa Njombe.