Mkoa wa Njombe
Mkoa wa Njombe ni mmojawapo kati ya mikoa mipya nchini Tanzania wenye postikodi namba 59000 [1], ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012[2]. Umepakana na mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya na Iringa.



Kutokana na hadhi mpya, wilaya ya Njombe imegawanyika kati ya ile ya mjini na ile ya vijijini. Pia, mwezi wa Machi 2012, imeanzishwa wilaya ya Wanging'ombe.
Mwaka 2012 katika eneo hilo kulikuwa na wakazi 702,097 Census 2012. Jalada kutoka ya awali juu ya March 5, 2016. Iliwekwa mnamo 14 February 2016. katika wilaya sita zifuatazo: Njombe Mjini (wakazi 130,233), Njombe Vijijini (wakazi 85,747), Makambako (wakazi 93,827), Makete (wakazi 97,266), Ludewa (wakazi 133,218), Wanging'ombe (wakazi 161,816).
Makao makuu yako Njombe mjini.
Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.
Kabila la Wabena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na wilaya ya Kilombero (Mkoa wa Morogoro), Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako katika wilaya ya Ludewa.
Yapo pia makabila madogo kama vile Wawanji, Wakisi, Wamanda, Wamagoma n.k. ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu Mkoani Njombe.
Karibu wakazi wote wa mkoa ni Wakristo, hasa Walutheri na Wakatoliki.
Majimbo ya bungeEdit
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Njombe Kaskazini : mbunge ni Joram Hongoli (CCM)
- Njombe Kusini : mbunge ni Edward Mwalongo (CCM)
- Makambako : mbunge ni Deo Kasenyenda Sanga (CCM)
- Wanging'ombe : mbunge ni Gerson Hosea Lwenge (CCM)
- Makete : mbunge ni Dk. Norman Adamson Sigalla (CCM)
- Ludewa : mbunge ni
Tazama piaEdit
TanbihiEdit
- ↑ https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/njombe.pdf[dead link]
- ↑ Staff. "Tanzania: State Gazettes New Regions, Districts", 9 March 2012. Archived from the original on August 23, 2012.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |