Utengule/Usongwe

(Elekezwa kutoka Utengule Usongwe)


Utengule/Usongwe ni kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Kijiji cha Utengule kiko kilomita 16 kutoka Mbeya mjini kupitia Mbalizi.

Kata ya Utengule/Usongwe
Kata ya Utengule/Usongwe is located in Tanzania
Kata ya Utengule/Usongwe
Kata ya Utengule/Usongwe

Mahali pa Utengule Usongwe katika Tanzania

Majiranukta: 8°40′47″S 33°51′35″E / 8.67972°S 33.85972°E / -8.67972; 33.85972
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbeya Vijijini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 55,082

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 55,082 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 41,952 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53208.

Mazingira ya Utengule pana mashamba ya kahawa na shamba kubwa ambalo ni mali ya Waswisi walioanzisha pia hoteli ya Utengule Country Club. Kuna kanisa na chuo cha Biblia cha Moravian.

Historia

hariri

Jina na mahali ni kihistoria; Utengule ilianzishwa na chifu Tovelamahamba Merere II wa Wasangu aliyepaswa kutoka Utengule Usangu baada ya kushambuliwa mara kwa mara na Wahehe chini ya Mkwawa. Alijenga Utengule mpya hapa Usafwa kwenye mtelemko wa mlima Mbeya mahali panapotazama bonde la mto Songwe. Utengule hii ya Merere II ilikuwa mji uliozungukwa na ukuta na sehemu za ukuta huu bado zinasimama kati ya mashamba na nyumba za kijiji. Merere akishirikiana na Wajerumani katika vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe na baada ya kifo cha Mkwawa Merere III alirudi Usangu alipojenga Utengule upya.

Kabla ya kuondoka Merere aliwahi kuwakaribisha wamisionari Wamoravian walioanzisha kituo cha nje ya mji wa Wasangu mwaka 1895 na kituo hiki cha Wamoravian kilikuwa kitovu kipya cha kijiji. Wamoravian walijenga kanisa, shule na karahana walipofundisha mafundi. Jengo la kanisa lipo hadi leo pamoja na chuo cha Biblia kinachosomesha wainjilisti wa Kanisa la Moravian Kusini Magharibi Tanzania (KMKMT). Askofu Mwafrika wa kwanza wa KMKMT Yohane Wawenza alikuwa mwenyeji wa Utengule.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-12.
  Kata za Wilaya ya Mbeya VijijiniMkoa wa Mbeya - Tanzania  

Bonde la Songwe | Igale | Igoma | Ihango | Ijombe | Ikukwa | Ilembo | Ilungu | Inyala | Isuto | Itawa | Itewe | Iwiji | Iwindi | Iyunga Mapinduzi | Izyira | Lwanjilo | Maendeleo | Mjele | Masoko | Mshewe | Nsalala | Santilya | Shizuvi | Swaya | Tembela | Ulenje | Utengule/Usongwe


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Utengule/Usongwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.