Uvimbe wa ubongo (kwa Kiingereza encephalitis) ni ugonjwa ambao husababisha ubongo kuvimba ghafla. Kwa kawaida husababishwa na virusi, bakteria (kwa Kiingereza Granulomatous amoebic encephalitis)[1], au vijidudu vingine. Kadiri ubongo unavyovimba, huweza kuharibiwa wakati unapokwaruzana na fuvu.

Picha inayoonyesha uvimbe katika ubongo.

Uvimbe wa ubongo unaweza kusababisha dalili hatarishi kama vile kupata kifafa na kiharusi, na hii inaweza kuwa mbaya zaidi.

Mwaka 2013, ugonjwa wa uvimbe wa ubongo uliua watu 77,000 duniani.

Ishara na dalili hariri

Kwa kawaida, watu wazima wenye ugonjwa wa uvimbe wa ubongo wana homa inayoanza ghafla, maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, na wakati mwingine kifafa. Watoto wadogo au watoto wachanga wanaweza kuwa na hasira, hawataki kula, na hupatwa na homa.

Kwa kawaida wagonjwa huwa wanachoka sana au wanachanganyikiwa.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uvimbe wa ubongo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.