Uwanja wa michezo wa Ellis Park

Uwanja wa michezo wa Ellis Park unafahamika pia kwa jina la Emirates Airline Park ni uwanja wa raga na shirikisho la mpira wa miguu katika jiji la Johannesburg, jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini. Mwaka 1995, fainali ya kombe la dunia ya raga ulichezwa katika uwanja huu ambapo timu ya taifa ya raga ya Afrika Kusini ndio walio ibuka washindi katika fainali hiyo. Uwanja huu ulikuwa wa kisasa zaidi kuliko zote baada ya maboresho ya mwaka 1982 na ulikuwa na uwezo wa kubeba washabiki takribani 60,000. Kwa sasa, uwanja huu unatumika kwa michezo ya raga na michezo ya soka na pia unatumika kwa matukio mengine kama vile matamasha

Ellis Park

Uwanja huu ulipewa jina hilo kutokana na mtu aliyetoa eneo la kujengwa na alifahamika kama J.D. Ellis. Rand milioni 450 ni kiasi kilichotolewa na kampuni ya Coca-Cola kubadili jina la uwanja kuwa Coca-Cola Park kati ya mwaka 2008 na 2012.[1]

Mechi za ligi, majimbo na ya kimataifa kwa mpira wa miguu zilichezwa katika uwanja huu na kushuhudia timu mbalimbali kama vile timu ya taifa ya Brazil, klabu ya Manchester United F.C na Arsenal F.C zikicheza Ellis Park.[2] [3]

Ellis Park ni uwanja wa nyumbani kwa timu zifuatazo:

  • Lions (Super Rugby) (Cats mpaka Septemba 2006) mashindano ya raga ya ukanda wa kusini.
  • Golden Lions, (Currie Cup) mashindano ya raga ya ndani ya nchi.

Michezo ya kriketi zilichezwa hapo awali katika uwanja huu. Michezo sita(6) za kriketi zilichezwa kati ya mwaka 1948 na 1954 kwenye uwanja wa Ellis Park.

Tangu uwanja wa michezo wa New Wanderers kufunguliwa mwaka 1956, Ellis Park haikuwahi kutumika kwa michezo ya daraja la kwanza ya kriketi na kwa sasa unatumika kwa michezo ya shirikisho la mpira wa miguu na raga.

Marejeo hariri

  1. "Ellis Park Stadium renamed to Coca-Cola Park" (Microsoft Word). Ellis Park Stadium (Pty) Limited. 4 July 2008. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 December 2008. Iliwekwa mnamo 9 October 2008.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "Archived copy". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 March 2010. Iliwekwa mnamo 9 May 2013.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. Johanesburg Stadium
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Ellis Park kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.