Valerie Aurora

Mwanasayansi wa kompyuta wa Marekani na mwanaharakati

Valerie Anita Aurora; ni mhandisi wa programu na mwanaharakati wa haki za wanawake.

Valerie Aurora

Alikuwa mwanzilishi wa Ada Initiative,[1] shirika ambalo lilitaka kuongeza ushiriki wa wanawake katika harakati za utamaduni na teknolojia.

Aurora pia anajulikana ndani ya jumuiya ya Linux kwa kutetea maendeleo mapya katika mifumo ya mafaili katika Linux, ikiwa ni pamoja na ChunkFS na Union mount. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Val Henson, lakini alilibadilisha muda mfupi kabla ya mwaka 2009, na kuchagua jina lake la kati kwa lile la mwanasayansi wa kompyuta Anita Borg. Mnamo mwaka 2012, Aurora, na mwanzilishi mwenza wa Ada Initiative Mary Gardiner, walitajwa kuwa watu wawili wenye ushawishi mkubwa katika usalama wa kompyuta na SC Magazine. Mnamo mwaka 2013, alishinda tuzo ya O'Reilly Open Source Award.

Marejeo

hariri
  1. "The Ada Initiative launches", LWN, February 7, 2011. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Valerie Aurora kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.