Victor Wanyama
Victor Mugubi Wanyama (Kenyan English: [ˈvɪktɜr muˈɡubiː wɑˈɲɑːmɑ] ( listen); alizaliwa 25 Juni 1991) ni mchezaji wa soka wa kulipwa wa Kenya ambaye anacheza kama kiungo wa kujihami kwa klabu ya Southampton na ni nahodha wa timu ya taifa ya Kenya.[1] Akiwa uwanjani, Wanyama, ni anajulikana kwa ajili ya sifa za uwanamichezo na za uongozi.[1]
Victor Wanyama | ||
Victor Wanyama 20170820.jpg | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Tarehe ya kuzaliwa | 25 Juni 1991 | |
Mahala pa kuzaliwa | Kenya, Kenya | |
Nafasi anayochezea | mchezaji wa soka | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Southampton | |
Timu ya taifa | ||
ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Kandanda ya Kenya | ||
* Magoli alioshinda |
Wanyama, ndiye Mkenya wa kwanza kabisa kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA wakati alipoifungia Celtic ilipoishinda Barcelona 2-1 tarehe 7 Novemba 2012.[2] Tarehe 11 Julai 2013, Wanyama, alielekea Ligi Kuu ya uingereza alipojiunga na klabu ya Southampton kwa £12.5 milioni hivyo basi kumfanya yeye kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa na klabu ya Scotland, kupita £9.5 milioni ambazo klabu cha Urusi cha Spartak Moscow kililipa kwa ajili ya kumsajili Aiden McGeady mwaka wa 2010.[3]
Tangu alipoanza kucheza kandanda ya kimataifa, Wanyama ameichezea timu ya taifa ya Kenya zaidi ya mara 30 kuanzia mwezi Mei 2007 akiwa na umri mdogo wa miaka 15.
Maisha ya mapema
haririWanyama alihudhuria Shule ya Upili ya Kamukunji, ambayo ina mafanikio sana na timu yake ya soka. Alipokamilisha masomo ya Sekondari, alichezea timu ya JMJ Academy kwa miaka mitatu wakati ambapo pia alijiunga na Ligi kuu ya Kenya na kuchezea vilabu vya Nairobi City Stars na AFC Leopards.[4] Mwaka 2007 alijiunga na klabu ya Allsvenskan na Helsingborg lakini baada ya kuondoka kwa nduguye McDonald Mariga ambaye alielekea Serie A na kujiunga la klabu cha Parma mwaka 2008, Wanyama, akarudi Kenya.
Wasifu wa klabu
haririBeerschot AC
haririBaada ya kufaulu katika majaribio, Wanyama, alisaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Beerschot AC katika majira ya joto ya 2008. Alichea mechi yake ya kwanza katika mechi ya mwisho ya msimu wa 2008-09. Mnamo Septemba 2009, Wanyama alitozwa faini ya €100 na kupewa marufuku ya kutocheza mechi tatu baada ya kumkabili kwa vurugu mchezaji Matias Suarez wa Anderlecht.[5]
Katika msimu wa joto wa 2010 klabu cha Ligi Kuu ya Scotland, Celtic ilijaribu kumsajili Wanyama, lakini Beerschot haikumruhusi kuondoka. Klabu ya CSKA Moscow ya Urusi pia kilijaribu lakini walishindwa.[6]
Wanyama, aliifungia Beerschot bao lake la kwanza tarehe 11 Desemba 2010, katika dakika ya 77 aliposawazisha dhidi ya Westerlo. Mnamo Aprili 2011, Alipokea marufuku nyingine ya kutocheza mechi 3 baada ya ushahidi wa video kuonyesha kuwa alimpiga kwa kisukusuku mchezaji Brecht Dejaeghere wa K. V. Kortrijk.[7]
Celtic
haririTarehe 9 julai 2011, hatimaye Wanyama, alikamilisha uhamisho alipo jiunga na Celtic kwa ada ya £900,000. Alisaini mkataba wa miaka minne na kwa kufanya hivyo akawa MKenya wa kwanza kucheza katika SPL. Wanyama alichagua nambari 67 kama heshima ya Lisbon lions, ambayo ilikuwa timu ya Celtic iliyoshinda Kombe la Ulaya la 1967 .[8][9] Wanyama, alichezea Celtic mechi yake ya kwanza ya ligi iliposhindwa 1-0 na St Johnstone tarehe 21 Agosti 2011.[10] Tarehe 29 Septemba 2011, alianza wakati Celtic ilitoka sare ya 1-1 na timu ya Italia Udinese kwenye Europa Ligi. Hii ilikuwa ni mechi yake ya kwanza ya Ulaya akiwa na klabu ya Celtic .[11] Tarehe 10 desemba 2011, Wanyama, aliifungia Celtic bao lake la kwanza katika ushindi wa1-0 dhidi ya Hearts katika Uga wa Celtic.
Mnamo Oktoba 2012, Wanyama, alifunga mara mbili dhidi ya St Mirren katika uga wa Saint Mirren.
Tarehe 25 oktoba 2012, wakala wa Wanyama alitoa taarifa ikisema kwamba Wanyama alikuwa akataa kuboresha mkataba wa Celtic, kwa madai kua Celtic haiwezi kukidhi mshahara wake huku kukiwa na uvumi wa mvuto kutoka kwa vilabu vya Uingereza. Tarehe 7 Novemba, Wanyama alifunga kwa kichwa bao la ufunguzi wakati Celtic ilipowashangaza Barcelona katika Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi kwa kuwalza mabao 2-1 katika uga wa Celtic[12]
Southampton
haririBaada ya uvumi mwingi kuvunjika kwa mazungumzo hapo awali, tarehe 11 Julai 2013, Wanyama, alisaini mkataba na kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza na Southampton kwa ada ya £12.5 milioni,[13] kumfanya kuwa Mkenya wa kwanza kuwahi kucheza katika Ligi Kuu ya Uingereza.[14]
Alicheza mechi yake ya kwanza Agosti 17, 2013, ugenini na kushinda 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion.[15] Wanyama, alicheza mechi 24 kwenye wake msimu wa kwanza, lakini majeraha yalizuia juhudi zake za kufanya mengi katika timu.[16]
Chini ya meneja mpya Ronald Koeman, Wanyama, aliboresha sana uchezaji wake. Maonyesho yake yalipeleka yeye kutunukiwa tuzo la Mchezaji bora wa Mwezi septemba.[17]
Wasifu wa kimataifa
haririWanyama, alicheza mechi yake ya kwanza kwa timu ya taifa ya Kenya Mei 2007, akiwa na umri wa miaka 15 tu katika mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria.[4] Pia alicheza mechi zote sita za Kenya za 2010 FIFA World Cup qualifiers. Alikuwa nahodha wa timu yake ya taifa katika mwaka 2013.
Kuonekana katika filamu
haririWanyama alishiriki katika uzalishaji wa filamu fupi kuhusu soka nchini Kenya iitwayo Mdudu Kijana, imeandikwa na kuongozwa na mwigizaji Ella Smith. [18]
Takwimu za wasifu
haririKlabu |
Msimu |
Ligi | Kikombe |
League Cup | Ulaya | Jumla | |||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kucheza |
Mabao |
Kucheza |
Mabao |
Mabao | Kucheza | Mabao | Kucheza | Mabao | |||
Beerschot AC | 2008–09 | 1 | 0 | – | – | – | – | – | – | 1 | 0 |
2009–10 | 20 | 0 | 1 | 0 | – | – | – | – | 21 | 0 | |
2010–11 | 30 | 2 | 4 | 0 | – | – | – | – | 34 | 2 | |
Jumla |
51 | 2 | 5 | 0 | – | – | – | – | 56 | 2 | |
Celtic | |||||||||||
2011–12 | 29 | 4 | 4 | 0 | 4 | 0 | 5 | 0 | 42 | 4 | |
2012–13 | 32 | 6 | 5 | 1 | 2 | 0 | 10 | 2 | 49 | 9 | |
Jumla |
61 | 10 | 9 | 1 | 6 | 0 | 15 | 2 | 91 | 13 | |
Southampton | |||||||||||
2013–14 | 23 | 0 | 1 | 0 | 0 | 0 | – | – | 24 | 0 | |
2014–15 | 32 | 3 | 2 | 0 | 4 | 0 | – | – | 38 | 3 | |
2015–16 | 25 | 1 | 2 | 0 | 0 | 0 | 3 | 0 | 30 | 1 | |
Jumla |
80 | 4 | 5 | 0 | 4 | 0 | 3 | 0 | 92 | 4 | |
Jumla |
194 | 16 | 17 | 1 | 10 | 0 | 18 | 2 | 239 | 19 |
Tuzo
haririKlabu
hariri- Ligi Kuu ya Scotland : 2011-12, 2012-13
- Kombe La Scotland : 2013
Binafsi
hariri- SPL Mchezaji bora kijana wa Mwaka: 2012-13
- SPL Mchezaji Kijana wa Mwezi: desemba 2011
Maisha binafsi
haririWanyamaa anatoka kwenye familia ya wanamichezo. Kaka yake McDonald Mariga anachezea Parma Fc, pia kama mchezaji wa kiungo cha kati,[19][20] Kaka zake wengine Thomas na Sylvester Wanyama, pia ni wachezaji katika Ligi ya Kenya. Baba yake, Noah Wanyama, alikuwa mchezaji wa AFC. Leopards katika miaka ya themanini(1980),[21] na dada yake Mercy ni mtaalamu wa mpira wa kikapu huko Marekani.[22]
Wanyama anasimamiwa na ExtraTime[23] na ana mkataba wa udhamini na Nike.[23]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "Celtic's Victor Wanyama has joined Southampton, say Kenyans". BBC Sport. 11 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Wanyama: Saints' sights on Europe". FIFA. 17 Desemba 2013. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Southampton in record swoop for Wanyama". FIFA. 11 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 Mugabe wants to cement position in Belgium club Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine. Standard Digital, 5 January 2010
- ↑ Wanyama suspendu trois matchs (Wanyama suspended three games) Archived 7 Oktoba 2012 at the Wayback Machine. Footgoal, 29 September 2009 (French)
- ↑ Wanyama va rester au Germinal Beerschot (Wanyama stays with Germinal Beerschot) Archived 19 Agosti 2010 at the Wayback Machine. Footgoal, 16 April 2010 (French)
- ↑ Wanyama poursuivi (Wanyama continued) Archived 7 Oktoba 2012 at the Wayback Machine. Footgoal, 18 April 2011 (French)
- ↑ "Stipe Pletikosa and Victor Wanyama set to make Celtic bow", Evening Times, Herald & Times Group, 20 July 2011. Retrieved on 23 September 2011.
- ↑ "Germinal's Victor Wanyama completes switch to Celtic", BBC Sport, 9 July 2011. Retrieved on 25 June 2012.
- ↑ "'When they scored the fans wanted more and we couldn't handle it’", Herald Scotland, Herald & Times Group, 23 August 2011. Retrieved on 30 August 2011.
- ↑ "Celtic 1–1 Udinese", BBC Sport, 29 September 2011. Retrieved on 29 September 2011.
- ↑ "Debutant Watt lights up memorable Celtic victory". UEFA. 25 Oktoba 2012. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Victor Wanyama: Southampton sign Celtic midfielder for £12.5m". BBC Sport. 11 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 11 Julai 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Wanyama makes Saints switch". Southampton FC. 11 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 11 Julai 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "West Brom 0–1 Southampton". BBC Sport. 17 Agosti 2013. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Victor Wanyama desperate for Saints to end with record breaking tally". Daily Echo. 21 Aprili 2014. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Wanyama considered switch" (24 October 2014). Football 411. Iliwekwa mnamo 2 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Film being made by Westcountry actor has celebrity support", Western Morning News, 2 July 2015. Retrieved on 5 March 2016.
- ↑ Mariga confirmed at Parma Archived 4 Machi 2012 at the Wayback Machine. Futaa.com, 31 January 2012
- ↑ Kenya's McDonald Mariga faces lengthy spell out BBC Sport, 13 April 2012
- ↑ Noah Wanyama hits the campaign trail Archived 4 Julai 2013 at the Wayback Machine. Futaa.com, 18 October 2011
- ↑ Mercy Wanyama secures Kshs.20Million scholarship package Archived 4 Januari 2019 at the Wayback Machine. MichezoAfrika, 6 August 2011
- ↑ 23.0 23.1 Victor Wanyama Archived 1 Julai 2012 at the Wayback Machine. ExtraTime
Viungo vya nje
hariri- Victor Wanyama career stats kwenye SoccerbaseSoccerbase
- Victor Wanyama at National-Football-Teams.com
Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Victor Wanyama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |