Kigunduzi moshi

(Elekezwa kutoka Vigunduzi moshi)

Kigunduzi moshi (kwa Kiingereza: smoke detector) ni kifaa kinachoweza kugundua moshi, ambao unaweza kuwa kiashiria cha moto.

Kigunduzi moshi ukutani.
Kigunduzi moshi kenye dari ya chumba.

Kuna mifumo miwili ya kimsingi:

  • kigunduzi moshi sahili kinawekwa mahali peke yake na inatoa sauti au kuwasha taa wakati hugundua moshi.
  • kigunduzi moshi kama sehemu ya mfumo wa usalama kinapeleka habari za moshi kwenda pameli inayowasha king’ora na kuchukua hatua za ziada, kama kuwasha vinyunyizo vya kuzima moto.

Teknolojia

hariri

Vigunduzi moshi hutumia moja kati ya mifumo miwili kutambua moshi:

Kigunduzi moshi kinuru

hariri

Kigunduzi moshi kinuru (optical smoke detector) huwa na kifaa cha kupima mabadiliko ya nuru wakati kuna moshi hewani. Hapo inatumia seli ya umemenuru inayopeka nuru kutoka diodi; moshi unafanywa na vipande vidogo vinavyoathiri kiwango cha nuru kinachofika kwenye seli.[1] Mwanga uliotumiwa unaweza kuwa wa infrared, mwanga unaoonekana, au ultraviolet . Hapo kigunduzi hugundua kuna mwanga mdogo. Chini ya mwangaza fulani, kigunduzi kinawasha king’ora.

Kigunduzi cha ioni

hariri

Kigunduzi cha ioni (ionization smoke detector) huwa na elementi nururifu ndani yake, kwa kawaida kiasi kidogo cha Ameriki. Vigunduzi hivyo huwa na chemba mbili ndani yake, moja iliyofungwa, nyingine iliyo wazi. Unururifu hutoa mionzi ya alfa inayoziionisha molekuli za hewa ndani ya kigunduzi na umeme unaweza kupita kwenye molekuli hizo. Kama moshi unaingia upande wa chemba iliyo wazi, sehemu za nyembe za alfa zitaathiri punje za moshi hewani badala ya molekuli za hewa. Hivyo volteji ya umeme katika chemba iliyo wazi inaanza kuwa tofauti na volteji katika chemba iliyofungwa. Tofauti hiyo inatambuliwa na kigunduzi na kufanya kiwashe king’ora.

Vigunduzi vya ioni hupatikana kwa bei nafuu kuliko vigunduzi vya nuru lakini husababisha pia king’ora cha uwongo zaidi kuliko vile vya nuru. [2] [3]

Marejeo

hariri
  1. Brazzell, D. "The Effects of High Air Velocity and Complex Airflow Patterns on Smoke Detector Performance" (PDF). AFCOM8-21.AFCOM-Miami-Admin.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-20. Iliwekwa mnamo 2009-05-13.
  2. Residential Smoke Alarm Performance, Thomas Cleary, Building and Fire Research Laboratory, National Institute of Standards and Technology, UL Smoke and Fire Dynamics Seminar. November, 2007.
  3. "Performance of Home Smoke Alarms Analysis of the Response of Several Available Technologies in Residential Fire Settings". Bukowski, Cleary et al. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-22.
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.