Kijiji

(Elekezwa kutoka Village)

Kijiji maana yake kwa Kiswahili ni mji mdogo. Kadiri ya mazingira, kinaweza kuwa na wakazi mia chache hadi elfu chache.

Kijiji cha Waberberi huko Ourika, Atlas, Moroko
Kijiji cha mbali huko Benin

Kwa kawaida vinapatikana mbali na miji, mashambani au porini kabisa.

Kijiji kama makazi ya wakulima

hariri

Kiasili idadi kubwa ya wanavijiji ni wakulima na asilimia ya wakazi wanaofanya kazi tofauti ni ndogo. Kihistoria watu wengu duniani waliishi katika vijiji na kujitegemea humo.

Katika nchi zilizoendelea kilimo kimebadilika na wakulima wamekuwa wachache wanaoendelea kulima mashamba yote kwa msaada wa mashine. Hapo wakazi wengine wa kijiji wanafanya kazi nje wakisafiri kila siku hadi mahali pa ofisi, duka au kiwanda.

Siku hizi kwenye Dunia kwa jumla wanadamu wanaoishi katika miji mikubwa ni wengi kuliko wale wanaoishi bado vjijini.

Kijiji kama kitengo cha utawala

hariri

Katika nchi nyingi kijiji ni pia ngazi ya chini ya utawala wa nchi. Kwa mfano nchini Tanzania kijiji kinajumlisha vitongoji kadhaa na pamoja a vijiji vingine inafanya kata.


Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: