Kipimo cha mjao

(Elekezwa kutoka Vizio vya ujazo)

Kipimo cha mjao (pia: kipimo cha ujazo, kizio cha ujazo) ni namna ya kutaja mjao au kiasi cha kiowevu (kwa mfano maji), gesi au vitu vya kumwaga kama unga au nafaka.

Ni pia kipimo cha kutaja nafasi ndani ya chombo, jengo au gimba la kijiometria kwa jumla.

Vipimo vya SI

hariri

Kipimo sanifu cha kimataifa cha mjao ni mita ya ujazo (alama m³) inayoweza kugawiwa kwa vizio vidogo kama vile desimita ya ujazo au sentimita ya ujazo; kwa kutaja mjao wa magimba makubwa ya maji kama vile ziwa au bahari uwingi wake ni kawaida kutumia uwingi wake yaani kilomita ya ujazo.

Kipimo cha kawaida cha kutaja viowevu kama maji, mafuta au kinywaji ni lita inayolingana na desimita ya ujazo.

Vipimo vya kimila

hariri

Kabla ya kuundwa kwa vipimo vya SI kulikuwa na vipimo mbalimbali vya mjao vilivyo tofauti kati ya nchi na nchi.

Vipimo vya Kiingereza

hariri

Hadi leo vipimo vya kiutamaduni vya Uingereza bado vinatumiwa katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza kama Marekani, Ufalme wa Maungano au Australia na hapo na pale kati ya watu wa nchi zilizokuwa koloni ya Uingereza. Ilhali vipimo vilisanifishwa katika Milki ya Uingereza wakati wa karne ya 19 baada ya Marekani kupata uhuru vipimo viko tofauti kidogo pande zote mbili. Mifumo hii miwli inajulikana kama "imperial units" (Uingereza) na "US customary measurement" (Marekani).

imperial gallon/US gallons
Marekani 231 in3 3.785412 lita
Ufalme wa Muungano 277.419 in3 4.54609 lita
Mjao (Uingereza)
Kizio Kifupi Ufafanuzi kipimo linganifu cha SI kipimo linganifu cha Marekani
Bushell 8 gal 36.37 L 9.606 US gal
Peck 2 gal 9.092 L 2.402 US gal
Gallon gal 4.54609 lita 1.201 US gal
Quart qt 14 gal 1.137 L 1.201 US qt
Pint pt 12 qt 568.3 ml 1.201 US pt
Gill 14 pt 142.1 ml 4.804 US fl oz
Fluid ounce fl oz 15 gill 28.41 ml 0.9608 US fl oz
Fluid drachm 18 fl oz 3.552 ml 0.9608 US drachm
Minim 160 fl dr 59.19 μl 0.9608 US minim


Mjao (Marekani)
Kizio Kifupi Ufafanuzi kipimo linganifu cha SI kipimo linganifu cha Uingereza
Gallon gal 231 cu in 3.785 L 0.8327 imp gal
Quart qt 14 gal 946.4 mL 0.8327 imp qt
Pint pt 12 qt 473.2 mL 0.8327 imp pt
Fluid ounce fl oz 116 pt 29.57 mL 1.041 imp fl oz
Fluid dram fl dr 18 fl oz 3.6967 mL 1.041 imp fl dr
Minim 160 fl dr 61.61 μL 1.041 imp fl minim

Vipimo vya Uswahilini

hariri

Waswahili wa kale kabla ya enzi ya ukoloni walikuwa na mfumo wa vipimo vyao, pia kwa mjao.

Katika biashara walipima hasa mjao wa nafaka. Kipimo cha kimsingi kilikuwa pishi, Pishi 1 iligawiwa kwa visaga 2 au vibaba 4.

Pishi 12 zilikuwa fara 1. Fara 5 au pishi 60 ziliitwa jizla 1, iliyoitwa pia mzo.[1]

Pishi ililingana takriban na lita 2.5 - 3 lakini jinsi ilivyo katika mazingira ya kimila vipimo vilitofautiana kati ya mji na mji au soko na soko.[2]

Marejeo

hariri
  1. Sehemu hii kuhusu vipimo vya waswahili inafuata maelezo katika kamusi ya Velten, Suaheli Wörterbuch Teil I, Suaheli - Deutsch, Berlin 1910, uk 358 ("pima")
  2. Kamusi ya Kiswahili Sanifu inataja kibaba kuwa "kipimo cha ujazo cha takriban gramu 700", kwa hiyo pishi 1 = vibaba 4 = gramu 2800. Haisemi ni gramu za nini; mahindi huwa na gramu 800 kwa lita moja, unga huwa na gramu ~500 kwa lita. Sacleux katika kamusi yake (dictionnaire Swahili Francais, 1939) anataja pishi kuwa sawa na nusu galoni ya Kiingereza yaani takriban lita 2.25. Velten katika kamusi yake (Suaheli Wörterbuch I. Teil, 1910; "pima") anataja pishi kuwa na takriban lita 4 akirejea kibaba kuwa kama lita 1; hapa ni juu mno kwa sababu kibaba kipo chini ya lita 1. Inawezekana ya kwamba tofauti kati ya kamusi zilizotajwa zinatokana na mahali tofauti ambako waandishi walikusanya habari zao.