Voice Of Youth Tanzania

Voice Of Youth Tanzania (kwa kifupi hujulikana kama VOYOTA; kwa Kiswahili: Sauti ya Vijana Tanzania) ni taasisi inayoshughulika na masuala ya vijana, wanawake na watoto. Ilianzishwa mwaka 2012 na Vincent Uhega [1] na kupata usajili mwaka 2017 [2]/

Voice of Youth Tanzania ni asasi isiyokuwa ya kiserikali na ambayo haijiendeshi kifaida yenye makao yake makuu mkoani Arusha katika mji mdogo wa Usa River ndani ya wilaya ya Arumeru.

Ni taasisi iliyoanza mara baada ya kumalizika kwa kampeni ya kusaka vipaji kwa vijana wa mtaani iliyojulikana kama Talanta Mtaani [3]

Malengo

hariri

Malengo yake ni kuuunga mkono juhudi za vijana kwa kukuza ustawi wa jamii kupitia utafiti, mafunzo ya ufundi, uwezeshaji wa kiuchumi, kukuza uelewa, mitandao na utetezi na sanaa zao.

Maono yake ni kuitengeneza jamii ya Watanzania yenye maono ya kufikia malengo yao.

Tanbihi

hariri
  1. https://oyaop.com/ambassador/vincent-uhega/
  2. IrishNet. ([2001]-). Ceolas. IrishNet. ISBN 0000000214. OCLC 556911737. {{cite book}}: Check |isbn= value: checksum (help); Check date values in: |date= (help)
  3. "Voice Of Youth Tanzania – Youth Empowerment for Sustainable Development" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-01-25.