Kujitolea

(Elekezwa kutoka Volunteering)

Kujitolea (katika Kiingereza:volunteering) ni kazi ambazo zinaweza kufanywa na mtu, kundi la watu, au taasisi yoyote bila ya kutarajia kupata malipo kutoka katika jamii au wale wanaowafanyia kazi hiyo[1].

Kujitolea huwa pia sehemu ya kuongeza na kukuza maarifa pamoja na kuendeleza matendo mema katika kuudhihirisha utu na ubinadamu, mtu anayejitolea mara nyingi hupata matokeo mazuri kutoka katika jamii yake, hasa ile anayoihudumia.[2]

Kujitolea pia hutumika kama sehemu ya mtu kutengeneza mazingira binafsi kwa ajili ya ajira yake ya baadaye, watu wengi wanaojitolea mara nyingi hupata mafunzo mbalimbali kwa sehemu waliyopo kama vile elimu, matibabu huduma za dharura na huduma nyingine kama vile kutoa huduma wakati wa majanga.

Kwa muktadha wa kijeshi, mtu anayejitolea ni yule anayejiunga na jeshi bila kuwa mwananchi ila mara nyingi huwa analipwa (mamluki).

Marejeo

hariri
  1. Wilson, John (2000). "Volunteering". Annual Review of Sociology. 26 (26): 215. doi:10.1146/annurev.soc.26.1.215.
  2. "Benefits of Volunteering". Corporation for National and Community Service. Iliwekwa mnamo 12 Aprili 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kujitolea kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.