Ujanseni

(Elekezwa kutoka Wajanseni)

Ujanseni ulikuwa tapo la teolojia ya Kanisa Katoliki (hasa nchini Ufaransa) katika karne ya 17 na ya 18. Tapo hilo lilisisitiza dhambi ya asili, uovu wa binadamu uliosababishwa nayo, haja ya neema ya Mungu na uteule kwa kudai linafuata mafundisho ya Augustino wa Hippo.

Cornelius Jansen (15851638), profesa wa Louvain (katika Ubelgiji wa leo).

Tapo lilitokana na vitabu vya mwanateolojia wa Uholanzi Cornelius Jansen vilivyochapishwa baada ya kifo chake (1638). Rafiki yake, abati Jean Duvergier de Hauranne, alisambaza mafundisho yake kwanza, na alipokufa yeye pia (1643) juhudi ziliendelezwa na Antoine Arnauld, lakini pia na Pierre Nicole, Blaise Pascal na Jean Racine.

Ujanseni ulipingwa na wengi, hasa Wajesuiti, kwa kuona unafanana na Ukalvini.[1]

Mwaka 1653, kwa hati Cum occasione, Papa Innocent X alilaani kama uzushi kauli tano za Wajanseni.[1] Viongozi wao walijaribu kulegeza msimamo wao bila kuachana nao kabisa, lakini hatimaye walihukumiwa tena na hati Unigenitus Dei Filius ya Papa Klementi XI mwaka 1713.[2]

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 Carraud, Vincent (2008-01-21) [Created 2007-06-20]. "Le jansénisme". Bibliothèque électronique de Port-Royal (lecture) (kwa French). Société des Amis de Port-Royal. ISSN 1776-0755. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-11. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link)
  2. Toon Quaghebeur, "The Reception of Unigenitus in the Faculty of Theology at Louvain, 1713-1719", Catholic Historical Review 93/2 (2007), pp. 265-299.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujanseni kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.