Abati (pia "abate") ni cheo cha mkuu wa monasteri yenye wamonaki wengiwengi (kwa kawaida 12 na zaidi) hasa katika Kanisa Katoliki.

Picha ya Kimisri ya Pakomi, mwanzilishi wa umonaki wa kijumuia.
Benedikto wa Nursia, akishika bakora na kanuni yake (Münsterschwarzach, Ujerumani).
Ngao ya abati asiye askofu, anayeongoza abasia ya kawaida. Ile ya abati anayeongoza abasia ya kijimbo ina kofia ya kijani.

Jina linatokana na Kilatini abbas, mkoko kutoka Kiaramu אבא (Abba, yaani "baba"). Kiongozi wa monasteri ya kike anaitwa pengine abesi.

Nchini Tanzania Wabenedikto wana maabati katima monasteri za Peramiho, Ndanda, Hanga na Mvimwa.

Maabati wachache wanapewa daraja takatifu ya askofu kwa kuwa monasteri yao ina jukumu la uchungaji kwa waamini wa eneo fulani (abasia ya kijimbo), kama ilivyokuwa kwa wale wa Peramiho na Ndanda wakati wa umisionari.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abati kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.