Kisiwa cha Wake
Kisiwa cha Wake ni atoli (aina ya kisiwa) katika Bahari ya Pasifiki, karibu na funguvisiwa la Hawaii. Inasimamiwa na Jeshi la Marekani. Ni eneo la ng'ambo la Marekani, ikihesabiwa kati ya Visiwa Vidogo vya Nje vya Marekani.
Kuanzia Desemba 1941 hadi Agosti 1945 atoli hiyo ilivamiwa na Milki ya Japani.
Jiografia
haririJinsi ilivyo na atoli nyingi, umbo la kisiwa ni takriban la duara; ukanda wa nchi kavu ni kama vipande kadhaa kwa hiyo tunaweza kusema atoli yote inafanywa na visiwa vitatu ambavyo kwa jumla huwa na eneo la hektari 737.06.
Kisiwa cha Wake kinahesabiwa kazi ya Visiwa vilivyo mbali kabisa na bara au na kisiwa chochote kingine. Visiwa vilivyo karibu ni Atoli ya Bohak (umbali km 560, hakuna watu) na Atoli ya Utirik (km 953, kuna watu) kwenye Visiwa vya Marshall kwa upande wa kusini-magharibi.
Wake iko km 2,416 upande wa mashariki wa Guam, km 3,698 upande wa magharibi wa Honolulu na km 3,204 upande wa kusini-mashariki wa Tokyo.
Wakazi
haririHakuna wakazi wa kudumu kwenye Kisiwa cha Wake, kwa hiyo hakuna shule ya watoto. Takriban watu 100 wanaishi huko wakati wowote. Wengi wao ni wakandarasi wanaotunza barabara, uwanja wa ndege na miundombinu mingine. [1]
Marejeo
hariri- ↑ "Top 10 Facts about Living Conditions on Wake Island", November 2, 2019. Retrieved on July 20, 2020.
Viungo vya Nje
hariri- Current Weather, Wake Island
- AirNav – Wake Island Airfield – Airport details, facilities and navigational aids
- Rocket launches at Wake Island (link broken)
- The Defense of Wake – United States Marine Corps historical monograph
- Surrender of Wake by the Japanese – Marines in World War II
- U.S. Army Strategic and Missile Defense Command Error in Webarchive template: Empty url. – Logistics, flight schedules, facilities
- Photographic history of the 1975 Vietnamese refugee camp on Wake Island
- Wake Island – Pacific Wreck Database
- Wake Island (1942) at the Internet Movie Database
- Wake Island: Alamo of the Pacific (2003) at the Internet Movie Database