Atolli ni kisiwa ambacho ni vipya vya matumbawe inayoonekana juu ya uso wa bahari. Mara nyingi umbo ni kama mviringo na kuna bwawa au wangwa wa maji katikati. Pia ukingo huu wa matumbawe umevunjika mara nyingi hivyo inaonekana kama mviringo wa visiwa vidogo na vyembamba.

Kutokea kwa atolii: jinsi matumbawe yanavyokua kando ya mlima unaozama chini

Karibu atolli zote za dunia ziko katika Pasifiki na katika Bahari Hindi. Atlantiki ina atolli chache katika bahari ya Karibi.

Neno atolli limetokana na lugha ya wenyeji wa Maldivi "atholhu". Limepokewa katika lugha ya Kiingereza likajulikana hasa kutokana na maandiko ya Charles Darwin aliyeeleza visiwa hivi kwa upana pamoja na nadhari jinsi zinavyokua.

Asili na kukua kwa atolli

hariri

Asili ya atolii huwa kisiwa cha volkeni kilichozama chini ya maji. Matumbawe yaliyokua kando ya kisiwa cha namna hiyo yanaendelea kustawi wakati kisiwa kinazama polepole sana. Hivyo atolli inaendelea kama mkasi wa kukua kwa matumbawe unalingana na mwendo wa kuzama kwa kisiwa chenyewe.

Kuna mifano ya atolli ambako kilele cha mlima wa katika bado inaonekana.

Atolli hatarini

hariri

Atolli nyingi za dunia ziko katika hatari ya kupotea kutokana na kupanda kwa uwiano wa bahari.

Mifano

hariri
  Makala hii kuhusu "Atolli" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Atolli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.