Wambundu
Wambundu ni kabila la Angola. Wanaishi katika maeneo ya Luanda, mji mkuu wa Angola, Malanje, na Bengo. Wako pia maeneo ya Cuanza Kaskazini na Cuanza Kusini. Lugha yao ni Kimbundu, ambayo ni lugha ya Kibantu.
Zamani Wambundu walikuwa wakaazi wa Ufalme wa Ndongo, uliokuwako kusini mwa Ufalme wa Kongo. Wafalme wa Ndongo waliitwa "ngolas", jina ambalo litapangiwa kwa taifa la kisasa la Angola Baadhi ya ngolas wanaojulikana zaidi ni:
Ngola KIluanji kia Ndambi, aliyetawala tangu mwaka 1562 hadi 1575
Njinga Ngola Kilombo kia Kaseda, aliyetawala tangu 1575 hadi 1592
Ngola Nzinga Mbandi (1592-1617)
Ana de Sousa Nzingha Mbandi (1624-1626)
Wambundu walishirikiana na Wazungu, hasa Wareno, katika Biashara ya watumwa waliosafirishwa toka Afrika mpaka Marekani.