Luanda (kirefu: São Paulo de Luanda: pia Loanda) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Angola ikiwa na wakazi 2,487,484 (katika rundu la jiji 7,805,000) wanaongezeka haraka kutoka ndani na nje ya nchi na ya bara la Afrika.

Jiji la Luanda
Nchi Angola
Mandhari kutoka juu
Luanda katika Angola
Luanda inavyoonekana kutoka angani

Jiografia

hariri

Mji wa Luanda uko mkoani Luanda, kaskazini ya mdomo wa mto Cuanza mwambaoni pa Atlantiki.

Historia

hariri

Mji ulianzishwa na Wareno mwaka 1575 BK kwa jina la São Paulo de Luanda. Umekuwa mji mkuu wa Angola tangu mwaka 1627.

Hadi mwaka 1850 Luanda ilikuwa kitovu cha biashara ya watumwa kwenda Brazil.

Wakati wa uhuru mwaka 1975 walowezi wengi Wareno waliondoka mjini. Vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Angola kati ya miaka 1974 - 2002 ilileta hasara pia kwa mji mkuu.

Wakazi

hariri

Kati ya wakazi, walio wengi kabisa ni Waafrika wa makabila kama vile Waovimbundu, Wakimbundu na Wakongo.

Lugha rasmi ni Kireno lakini lugha nyingi za Kibantu zinatumika pia.

Uchumi

hariri

Luanda ni bandari muhimu nchini pia mwanzo wa reli kwenda Malange.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Luanda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.