Wiki ya Usomaji Ramani

Wiki ya Usomaji Ramani nchini Uingereza (kwa Kiingereza National Map Reading Week) ni wiki iliyobuniwa na "Ordinance Survey", ambayo ni ofisi ya upimaji na ramani katika Ufalme wa Muungano, kwa shabaha ya kuhamasisha watu kujifunza namna ya kusoma ramani. Wiki hiyo huadhimishwa wiki ya tatu ya mwezi Oktoba. [1]

Malengo makubwa ya wiki hiyo ni kuhamasisha umma na jamii katika matumizi na huduma za ramani [2] Kulingana na utafiti wa mwanzo iligundulika kuwa raia wengi walishindwa kuonyesha miji ya London na Birmingham kwenye ramani ya nchi.[3]

Wasiwasi wa watu wengi kupoteza maarifa ya usomaji ramani haukuwa jambo jipya, kulingana na utafiti wa maktaba ya Uingereza ulionyeshwa na mchorakatuni aitwaye John Brian Hartley kufikia mwaka 1980 wasiwasi wa upoteaji wa maarifa ya asili ya usomaji ramani ulianza kutoweka baada ya uvumbuzi na ugunduzi wa maarifa ya ramani katika mfumo wa kidijitali kuanza kukua [4].

Marejeo hariri

  1. "Back on the map: Why paper sometimes isn’t enough to help you find your way", 27 October 2016. Retrieved on 29 November 2016. 
  2. "OS #GetOutside: Map Reading Week 2016". Iliwekwa mnamo 21 September 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "The Scilly Isles? Is that in Scotland", Telegraph, 21 September 2016. Retrieved on 21 September 2016. 
  4. "Map Reading in the 20th Century". British Library. British Library. Iliwekwa mnamo 20 October 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya Nje hariri