Wikipedia:Makala ya wiki/Mbaraka Mwinshehe
Mbaraka Mwinshehe Mwaruka (27 Juni 1944 - 12 Januari 1979) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania.Mbaraka Mwinshehe Mwaruka alizaliwa mjini Morogoro 27 Juni, 1944. Mbaraka Mwinshehe alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa katika watoto 12 . Baba yake Mzee Mwinshehe Mwaruka alikuwa Mlugulu msomi na karani katika mashamba ya katani, na mama yake alikuwa Mngoni. Kati ya hao kumi na mbili, ni yeye na wadogo zake Zanda na Matata ndio walikuwa wanamuziki, Zanda alikuwa mwimbaji, akiimba pia nyimbo za kizungu katika bendi ya Morogoro na Matata alikuwa mpiga drum pia bendi hiyohiyo. Kutokana maelezo ya familia, babu yake Mbaraka alikuwa wa kabila la Wadoe wa Bagamoyo na alipelekwa Mzenga (Kisarawe) akawe chifu wa huko na wakoloni. ►Soma zaidi