Wikipedia:Makala ya wiki/Virusi
Virusi (kutoka Kilatini virus, yaani "sumu“) ni chembe ndogo sana iliyoundwa na maada jenetiki, kama ADN au ARN, katika koti la proteini. Vinaweza kusababisha magonjwa.
Jinsi ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi
Unashauriwa:
- kunawa mikono mara kwa mara angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo, tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
- usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
- epuka kuwa karibu sana na wagonjwa
- wakati ugonjwa unazuru katika nchi ulipo, epuka kusalimu wengine kwa kushikana mikono
- kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga yako ni dhaifu katika hali hii)
- tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya chooni / toilet paper) na uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
- safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombe, deski, simu yako)[1]; kama unayo, tumia dawa ya alikoholi (spirit – si konyagi!), lowesha karatasi nayo, futa, tupa ►Soma zaidi
- ↑ About prevention and treatment, tovuti ya National Center for Immunization and Respiratory Diseases (NCIRD), Division of Viral Diseases, Marekani, iliangaliwa 30 Januari 2020