Wilaya ya Kibiti ni wilaya mpya katika Mkoa wa Pwani iliyoanzishwa mnamo mwaka 2015. Maeneo yake yalitengwa na Wilaya ya Rufiji.

Kulingana na matokeo ya sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilikadiriwa kuwa 133,727 kwa mwaka 2016. [1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 195,638 [2].

Misimbo ya Posta katika wilaya hii huanza kwa namba 616.

Wilaya ya Kibiti inajumlisha ndani yake kata za delta ya mto Rufiji ambazo hazijafikiwa bado na maendeleo ya miundombinu hadi mwaka 2017.

Kata na Wakazi hariri

Wilaya ya Kibiti ilikadiriwa kuwa na wakazi 133,727 mnamo mwaka 2016.

Kata zake zilikuwa na wakazi wafuatao:

Tanbihi hariri

  1. Makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016, uk. 56; tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, iliangaliwa Juni 2017
  2. https://www.nbs.go.tz

Viungo vya Nje hariri

  Kata za Wilaya ya Kibiti - Mkoa wa Pwani - Tanzania
 

Bungu | Dimani | Kibiti | Kiongoroni | Mahege | Maparoni | Mbuchi | Mchukwi | Mjawa | Mlanzi | Msala | Mtawanya | Mtunda | Mwambao | Ruaruke | Salale


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kibiti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.