Magamba Kwalukonge

4°57′00″S 38°10′08″E / 4.9501°S 38.1689°E / -4.9501; 38.1689

Kwa matumizi mengine ya jina hili, tazama Magamba.

Magamba Kwalukonge ni kata ya Wilaya ya Korogwe Vijijini katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,108 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,314 waishio humo.

Msimbo wa posta ni 21622.

Magamba Kwalukonge iko takriban kilomita 12 kusini magharibi kwa Mombo, hivyo karibu na barabara kuu Tanga - Moshi. Upande wa kusini eneo lake linavuka mto Pangani.

Kata hiyo inaundwa na vijiji vitatu ambayo ni Makole, Changalikwa pamoja na Magamba.

Kwalukonge Magamba inapakana na kijiji cha Makole upande wa kaskazini magharibi na mlima Mafi upande wa magharibi.

Kuna shule moja ya msingi na shule ya sekondari iitwayo Mkalamo ambayo imeanzishwa mwaka 2003 na shule hii inachukua wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba kutoka katika shule ya msingi Magamba.

Kijiji cha Kwalukonge - Magamba kilishawahi kushika ushindi mbalimbali wa kiserikali wakati nchi ya Tanzania bado ilikuwa inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kijiji hiki kimezungukwa na mikonge pande zote nne za dunia.

Mazao yanayolimwa katika kijiji cha Kwalukonge ni mahindi, maharage, kunde, mihogo na karanga. Hivi karibuni zao la ngwasha limekuwa likilimwa kama zao la biashara na limekuwa likileta kipato kikubwa kwa wanakijiji waishio maeneo hayo. Wanakijiji wa Kwalukonge wanaishi kijamaa ambapo hutegemea katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile mazishi, ngoma, sherehe na mambo mengine ya kijamiii.

Shughuli za kijamaa katika kijiji cha Kwalukonge zilianzishwa na marehemu Adam Philipo Mwilongo pamoja na wazee wengine ambao waliamua kuanzisha ushirika (mfumo wa ujamaa) ambao unahusisha shughuli za maendeleo zaidi na kuanzisha miradi mbalimbali.

Changamoto ya uhaba wa maji kwa hii miaka ya karibuni imekikumba kijiji cha Kwalukonge kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea. Hivyo wanakijiji wanafanya jitihada tofauti ili kuhakikisha wanakabiliana nayo na pia kushawishi serikali kusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Korogwe Vijijini - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Bungu | Chekelei | Dindira | Foroforo | Hale | Kalalani | Kerenge | Kizara | Kwagunda | Kwashemshi | Lewa | Lutindi | Magamba Kwalukonge | Magila Gereza | Magoma | Makumba | Makuyuni | Mashewa | Mazinde | Mgwashi | Mkalamo | Mkomazi | Mkumbara | Mlungui | Mnyuzi | Mombo | Mpale | Mswaha | Vugiri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Magamba Kwalukonge kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.