Wilaya ya Nandi
Wilaya ya Nandi ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Wilaya ya Nandi | |
Mahali pa Wilaya ya Nandi katika Kenya | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Mji mkuu | Kapsabet |
Eneo | |
- Jumla | 2,884.5 km² |
Idadi ya wakazi (2009 Sensa[1]) | |
- Wakazi kwa ujumla | 752,965 |
Makao makuu yalikuwa mjini Kapsabet.
Kwa sasa imekuwa kaunti ya Nandi.
Wilaya hii ilikuwa na jumla ya wakazi 578,751 (sensa ya 1999) [1] Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine..
Maumbile ya wilaya hii yamejawa na Milima ya Nandi. Wenyeji ni haswa wa kabila la Wanandi.
Wilaya ya Nandi ni maarufu kwa kuwa nyumbani kwa Wakenya wakimbiaji wengi, wakiwemo Kipchoge Keino, Henry Rono, Moses Tanui na Bernard Lagat.
Serikali za Mitaa
haririSerikali ya Mtaa | Aina | Idadi ya Watu | Wakaazi wa mjini* |
---|---|---|---|
Kapsabet | Manispaa | 64,830 | 17,918 |
Nandi Hills | Mji | 63,134 | 3,575 |
Nandi county | Baraza la Mji | 450,787 | 3,156 |
Maeneo ya utawala
haririTarafa | Idadi ya Watu | Wakazi wa mjini* | Makao makuu |
---|---|---|---|
Aldai | 96,220 | 200 | Kobujoi |
Kabiyet | 43,367 | 751 | Kabiyet |
Kapsabet | 125,115 | 16,942 | Kapsabet |
Kaptumo | 26,782 | 150 | Kaptumo |
Kilibwoni | 62,692 | 116 | Kilibwoni |
Kipkaren | 52,753 | 0 | |
Kosirai | 35,383 | 957 | |
Nandi Hills | 77,514 | 3499 | Nandi Hills |
Tinderet | 58,925 | 0 |
Maeneo Bunge
haririWilaya hii ilikuwa na Maeneo Bunge manne: