William Tanui
William Kiptarus Tanui (alizaliwa 22 Februari 1964) alikuwa mwanariadha wa Kenya ambaye alishinda nishani katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 1992.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Men’s Wanariadha | ||
Anawakilisha nchi Kenya | ||
Olympic Games | ||
Dhahabu | 1992 Barcelona | 800 metres |
All-Africa Games | ||
Dhahabu | 1991 Cairo | 800 metres |
Historia yake
haririAlizaliwa katika kaunti ya Nandi nchini Kenya. Alikuja kugundua talanta yake baada ya muda mrefu, wakati alishinda mbio za mita 1500 katika majaribio ya Kenya ya Mashindano ya Jumuia ya Madola mnamo 1989, lakini akaibuka wa sita katika mashindano hayo mnamo 1990 jijini Auckland, New Zealand.
Mwaka huohuo, alishinda mbio za mita 800 katika Mashindano ya Afrika Mashariki jijini Cairo. Katika mashindano ya ndani ya Dunia jijini Seville mnamo 1991, Tanui alimaliza wa kwanza lakini ushindi huo ukafutwa kwa kutoka leni yake mapema. Alishinda mbio za mita 800 katika Michezo ya All-Africa ya 1991.
Fursa yake kuu iliwadia wakati wa Mashindano ya Olimpiki ya 1992 jijini Barcelona. Katika fainali ya shindano la mita 800 alishinda dhahabu huku akimaliza katika leni ya tatu na kumshinda mwenziwe Nixon Kiprotich kwa karibu.
Hata hivyo alimaliza wa nane katika Mashindano ya IAAF ya 1003 jijini Stuttgart ambapo alimaliza wa saba.
Pia alimaliza wa pili katika Kombe la Dunia la IAAF, mbio za mita 800 mnamo 1992 na 1994[1].
Hatima ya kazi yake
haririTanui alijishughulisha zaidi na mbio za mita 1500 kuliko zile za mita 800 katika siku za baadaye za kazi yake.
Alimaliza wa tano katika mbio hizo wakati wa Mashindano ya Olimpiki ya 1996 jijini Atlanta (Georgia). Katika mashindano ya Ndani ya Dunia, Tanui alimaliza wa tatu katika shindano la m 1500 jijini Paris mnamo 1997, na wa nne kule Maebashi mnamo 1999.
Sasa hivi Tanui hujitolea kwa Jamii ya Terik kuikuza miradi ya Michezo kwa machipukizi.
Marejeo
hariri- ↑ gbrathletics.com: IAAF WORLD CUP IN ATHLETICS
Viungo vya nje
hariri- terik.org *IAAF wasifu wa William Tanui