Wilton Daniel Gregory
Wilton Daniel Gregory (amezaliwa 7 Desemba 1947) ni askofu wa Kanisa Katoliki la Marekani ambaye amehudumu kama Askofu Mkuu wa Washington tangu 2019. Papa Fransisko alimpandisha hadi cheo cha kardinali mnamo Novemba 28, 2020, na kumfanya kuwa kardinali wa kwanza Mwafrika-Amerika.[1]
Gregory hapo awali aliwahi kuwa askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Chicago kuanzia 1983 hadi 1994; kama Askofu wa Belleville kuanzia 1994 hadi 2004; na kama Askofu Mkuu wa Atlanta kutoka 2005 hadi 2019. Alikuwa rais wa kwanza Mweusi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, akihudumu kutoka 2001 hadi 2004.[2]
Marejeo
hariri- ↑ Horowitz, Jason. "Pope Francis Appoints First African-American Cardinal", The New York Times, October 25, 2020.
- ↑ "The Most Reverend Wilton D. Gregory", Roman Catholic Archdiocese of Atlanta.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |