Yakobo Berthieu, S.J. (Polminhac, Cantal, Ufaransa, 27 Novemba 1838 - Ambiatibe, Madagaska, 8 Juni 1896) alikuwa padri na mmisionari Mjesuiti nchini Madagaska [1].

Picha halisi ya Mt. Yakobo Berthieu.

Wakati wa amani na vilevile wakati wa vita alijitosa kueneza Injili, na kisha kufukuzwa mara tatu kutoka misheni yake, alipigwa mateke na kudaiwa aasi dini ya Kikristo, hatimaye aliuawa kwa chuki dhidi ya imani hiyo katika Uasi wa Menalamba mwaka 1896, akipata hivyo kuwa mfiadini.

Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 17 Oktoba 1965 na Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 2012 wa kwanza kutoka nchi hiyo.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Juni[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

  • Boudou, A., J. Berthieu, Paris, 1935
  • Blot, B., He loved to the end, Fianarantsoa, 1965.
  • Sartre, Victor, Blessed Jacques Berthieu, martyr Madagascar, Lille, 1996.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.