Zama za Chuma

(Elekezwa kutoka Zama za chuma)

Zama za Chuma katika historia kilikuwa kipindi kirefu baada ya watu kuanza kutumia vifaa vya chuma. Kabla yake, walikuwa wakitumia vifaa vya shaba na awali mawe yaliyochongwa tu.

Vifaa vya chuma

Sehemu nyingi za Ulaya, Afrika na Asia walifikia Zama hizi za Chuma kunako mwaka wa 500 KK. Kwa upande wa Ulaya, ni kipindi cha kabla ya historia, kwa sababu watu wa Zama za Chuma hawakuwa wakiandika kumbukumbu zao.

Uhunzi hariri

Chuma ni rahisi kukipata, lakini ni vigumu sana kukitengenezea vifaa. Inabidi kukiyeyusha kwa halijoto ya juu kuliko shaba. Watu waliojifunza namna ya kutengeneza vifaa kwa kutumia chuma walikuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi sana kwa vyuma hivyo.

Hii inamaanisha kwamba tabia za watu hubadilika. Kwa mfano, watu wengi wana uwezo zaidi wa kumiliki jembe la chuma. Wameweza kulima mashamba yao vizuri na mazao kukua vyema kabisa.

Baadhi ya watu walibuni sarafu ili kusaidia kununua na kuuza mazao yao na vifaa vyao vya chuma.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zama za Chuma kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.