Zineb El Rhazoui
Mwandishi wa habari wa Ufaransa
Zineb El Rhazoui (kwa Kiarabu: زينب الغزوي, Zainab al-Ghazwi; alizaliwa Moroko, 19 Januari 1982) ni mwandishi wa habari nchini Ufaransa.
Zineb El Rhazoui | |
Zineb El Rhazoui mwaka 2017 | |
Nchi | Moroko |
---|---|
Kazi yake | mwandishi wa habari |
Alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti lenye maudhui ya kejeli Charlie Hebdo lenye makao makuu mjini Paris kuanzia 2011 hadi 2017.[1] Alikuwa Moroko wakati wa mauaji ya Charlie Hebdo tarehe 7 Januari 2015.
Alikuwa mtaalamu wa dini na mkosoaji wa dini ya Uislamu[2] kupitia uandishi wa magazeti. Tangu kutokea kwa mauaji aliamua kuwa mwanaharakati wa kidini na haki za binadamu,[3] kuongea hadharani ulimwenguni kote na kwenye majukwaa kwa kuizunguka dunia kuhusu Uislamu na uhuru wa kujieleza.
Marejeo
hariri- ↑ "Charlie Hebdo: first cover since terror attack depicts prophet Muhammad". the Guardian (kwa Kiingereza). 2015-01-13. Iliwekwa mnamo 2022-03-01.
- ↑ http://www.aftenposten.no/amagasinet/Zineb-El-Rhazoui-fortsetter-kampen-for-ytringsfriheten-i-Charlie-Hebdo-7957936.html
- ↑ "Isis supporters call for Charlie Hebdo survivor Zineb el-Rhazoui to be murdered by terrorist lone wolves". International Business Times UK (kwa Kiingereza). 2015-02-19. Iliwekwa mnamo 2022-03-01.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zineb El Rhazoui kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |