Ab Urbe condita (kifupi: A.U.c. AUC, AVC, a.U.c. hata AU) ilikuwa namna ya Waroma wa Kale kuhesabu miaka. Maneno hayo ni ya Kilatini na yanamaanisha "tangu kuundwa kwa mji". Kwa hiyo Waroma wa Kale walihesabu miaka tangu kuundwa kwa mji wa Roma. Tendo hili liliaminiwa kutokea mwaka 753 KK iliyohesabiwa kuwa mwaka A.U.c. 1.

Haikuwa hesabu pekee katika Roma ya Kale; kwa kawaida walitaja mwaka kwa kutumia majina ya makonsuli wawili waliochaguliwa pamoja kuongoza serikali kwa mwaka mmoja.

Tarehe halisi ya kuundwa kwa Roma haijulikani. Mwanahistoria Mroma Marcus Terentius Varro alikadiria tarehe inayolingana na 21 Aprili 753 KK kuwa siku ambako mji wa Roma uliundwa.

Kutafsiri miaka A.U.c. kwa miaka ya Kalenda ya Gregori

hariri

Fomula

hariri

Miaka kabla ya kuundwa kwa Roma (ante Urbem conditam) hukadiriwa hivyo:

  • Mwaka   ante u. c. ni mwaka   KK
  • Mwaka   KK ni mwaka   ante U. c.

Miaka baada ya kuundwa kwa Roma (ab Urbe condita) na kabla ya kuzaliwa kwa Kristo hukadiriwa hivyo:

  • Mwaka   a. u. c. ni mwaka   KK
  • Mwaka   KK ni mwaka   a. U. c.

Baada ya kuzaliwa kwa Kristo:

  • Mwaka   a. U. c. ni mwaka   BK
  • Mwaka   BK ni mwaka   a. U. c.

Mifano

hariri
Mwaka 440 kabla ya kuundwa kwa Roma (ante Urbem conditam) = 440 + 753 = 1193 KK (mwaka ulioaminiwa uharibifu wa Troia ulitokea)
245 a. U. c. = 754−245 = 509 KK (mwanzo wa Jamhuri ya Roma)
2 ante Urbem conditam = 755 KK
1 ante Urbem conditam = 754 KK
1 ab Urbe condita = 753 kabla ya Kristo (mwaka wa kuundwa kwa mji wa Roma)
2 a. U. c. = 752 KK
usw.
750 a. U. c. = 4 KK (mwaka wa kifo cha Herode Mkuu);
751 a. U. c. = 3 KK;
752 a. U. c. = 2 KK;
753 a. U. c. = 1 KK;
754 a. U. c. = 1 baada ya Kristo;
755 a. U. c. = 2 BK
2777 a. U. c. = 2024 BK
na kadhalika