Abominable (filamu ya 2019)

2019 filamu iliyoongozwa na Jill Culton na Todd Wilderman

Abominable ni filamu ya matukio ya uhuishaji iliyoachiwa mwaka 2019 na kutayarishwa na DreamWorks Animation na Pearl Studio, iliandikwa na kuongozwa na Jill Culton akiwa na msaidizi wake Todd Wilderman, na waigiza sauti Chloe Bennet, Albert Tsai, Tenzing Norgay Trainor, Eddie Izzard, Sarah Paulson, Tsai Chin, na Michelle Wong.

Abominable (filamu ya 2019)
Imetayarishwa na Suzanne Buirgy
Peilin Chou
Nchi
  • United States
  • China
Lugha English

Filamu hiyo inamuelezea msichana anayeitwa Yi, ambaye anakutana na Yeti mdogo juu ya paa la ghorofa lao huko Shanghai, na kumpa jina la Everest na kuanza jitihada kubwa ya kumuunganisha kiumbe huyo wa kichawi na familia yake katika sehemu ya juu zaidi duniani akiwa na zake marafiki wakorofi Jin na Peng, lakini marafiki hao watatu watalazimika kukaa hatua moja mbele ya Burnish,ambae ni tajiri mwenye nia ya kukamata Yeti, akiwa na mtaalamu wa wanyama Dk. Zara.

Filamu hii ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Toronto mnamo 7 Septemba 2019, na iliachiliwa na Universal Pictures nchini Marekani mnamo 27 Septemba [1] [2] [3] huku Pearl Studio ikisambaza filamu hiyo nchini China. [4]

Filamu hiyo ilipokewa kwa maoni chanya kutoka kwa wachambuaji wa filamu na imeingiza zaidi ya dola za Kimarekani milioni 188 kote ulimwenguni. Katika Kusini-mashariki mwa Asia, Abominable imepata utata kwa tukio linalohusisha ramani ya eneo hilo na laini ya dashi tisa, njia ya kuweka mipaka inayopingwa inayotumiwa na Jamhuri ya Watu wa China kudai sehemu ya Bahari ya Kusini ya China. Kutokana na hili, filamu hiyo imepigwa marufuku katika nchi kadhaa zinazohusika katika mizozo ya kimaeneo na China kuhusu Bahari hiyo, yaani, Ufilipino, Vietnam na Malaysia.

Muendelezo wa filamu hii, Abominable and the Invisible City, ulitolewa kwenye huduma za utayarishaji wa filamu Peacock na Hulu mnamo Oktoba 2022.

 Marejeo

hariri
  1. "Universal Delays DreamWorks Animation's 'How to Train Your Dragon 3,' Sets 'Everest' Feature". Animation World Network. Desemba 7, 2016. Iliwekwa mnamo Julai 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Brendon Connelly (23 Machi 2017). "What's going on at DreamWorks Animation?". Den of Geek. Iliwekwa mnamo Februari 11, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Abominable". Universal Pictures. Iliwekwa mnamo 22 Februari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "'Abominable': All Yeti for the Big Screen", September 8, 2019. 
  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abominable (filamu ya 2019) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.