Ahmad Basheikh Husein
Ahmad Basheikh Husein (Mombasa, 1909 - Mombasa, 11 Desemba 1961) alikuwa mshairi na mwandishi katika usultani wa Mombasa. Aliandika ushairi na hadithi zake kwa Kiswahili. Aliandika vitabu vyake kwa sultani wa Mombasa.
Ahmad Basheikh Hussein | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Ahmad Basheikh Hussein |
Alizaliwa | 1909 |
Alikufa | 11 Desemba 1961 |
Nchi | Kenya, Mombasa |
Kazi yake | Mshairi,Mwalimu wa Quran |
Alijulikana kutunga na kuandika mashairi mengi kama Kunena nawe sikomi, Mbasi, Wanawake, Ila kafati shuarai au Tumi Nakutuma. Ustadh Ahmad Basheikh Bin Hussein alikua pia mwalimu wa Quran na msomi mkubwa wa dini uhodari wake katika usomaji wa Quran pamoja na sauti yake nyororo ulivutia wasikilizaji wake nchini Kenya,Tanzania na hata Afrika ya kati ikiwemo nchi za Congo
Alikuwa mwana wa Basheikh Hussein na Bibi wa Mwinyi Matano. Alikuwa mjomba wa mshairi Ahmad Nassir Juma Bhalo ambaye ndiye aliyeandika mistari na mashairi yake pamoja na Msomi na mwanasiasa maarufu mombasa sheikh Abdullah Nassir Juma Bhalo.
Ahmad Basheikh Hussein alijulikana kwa jina la (Kibwana)jina alilopewa kwa heshima aliyokuwa nayo wakati huo.
Ustadh Ahmad Basheikh Bin Hussein alimuowa Sharriffa Haji Fazil Murad na kujaliwa nae watoto ambao ni malenga maarufu Maalim Basheikh Ahmad Basheikh Bin Hussein pamoja na Fadhil Ahmad Basheikh Bin Hussein, Shufaa Ahmad Basheikh Bin Hussein na wengine Ustadh Ahmad Basheikh Bin Hussein pia ni babu wa Awadh Basheikh maarufu kama Mwana wa Kanga.
Ahmad Basheikh Bin Hussein ni Mlezi wa Mtunzi wa Sauti ya Dhiki Mwalimu Abdulatif Abdalla ambaye ni Babu yake.
Ustadh Basheikh alivuta pumzi zake za mwisho wakati akisoma Quran tukufu Disemba 11 mwaka 1961 katika Kituo cha redio cha Sauti ya Mvita
Mashairi yake
hariri- Kunena nawe sikomi
- Mbasi
- Wanawake
- Ila kafati shuarai
- Tumi Nakutuma
- Mahaba Matungu
- Mahaba si tamu
- Wake kwa waume
- Usia kwa mke mwana
- Asiyetaka kufunzwa
- Taa yetu ya thureya imezimika ghafula kifo cha Mbarak Ali Hinawi
- Mimi sina neno huba zimekwisha
Mistari ya Mimi sina neno huba zimekwisha
haririLipi kuu mno ~ la kunionesha.
Ni mangi maneno ~ na kuhakikisha
Mimi sina neno ~ huba zimekwisha.
Hiyo siyo ndiya ~ ya kuridhi moyo
Watu wakutaya ~ kwa uyafanyayo
Walaje pamoya ~ na mume mwenziyo.
Marejeo
hariri- Knappert, J. (1982). Four Centuries of Swahili Verse.
- Frankl, P. J. (1991). Mombasa under the BuSaʿidi A Leaf from the Taylor Papers (SOAS MS 47757, folio 50). Zeitschrift der Deutschen Morgenländischen Gesellschaft, 141(1), 131-138.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahmad Basheikh Husein kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |