Mjomba ni jina ambalo mtoto (wa kiume au wa kike) anamuita mwanamume ambaye ni ndugu (mkubwa au mdogo kwa umri) wa mama yake. Upande wa pili, mjomba anamuita mtoto huyo "mpwa".

Ukilinganisha na lugha za Ulaya, zile za Kibantu zinazingatia zaidi umri na hasa jinsia za wazazi na ndugu zao. Hivyo, kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" (ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi).

Hivyo, anayeitwa kwa Kiingereza "uncle" anaweza akaitwa kwa Kiswahili "mjomba", lakini "baba mkubwa" (kama ni kaka wa baba) au "baba mdogo" (kama ni mdogo wa baba). Vilevile neno "aunt" linaweza kumaanisha "shangazi" (dada wa baba), "mama mkubwa" (kama ni mkubwa wa mama) au "mama mdogo" (kama ni mdogo wa mama).

Tena kwa Kiingereza "nephew" linaweza kumaanisha "mpwa" lakini pia "mtoto" (ikiwa anayesema ni wa jinsia ileile ya mzazi).

Wajibu na haki kati ya mjomba na mpwa wake vinategemea utamaduni wa mahali. Katika baadhi ya makabila, kama yale yanayotia maanani ukoo wa mama kuliko ule wa baba ("mfumojike" au "mfumomama"), mjomba ni muhimu kuliko baba mzazi.

Pengine kwa heshima mtu anaweza akamuita mwingine "mjomba" ingawa hawana undugu wowote wa karibu.

Mke wa mjomba anaitwa "mkazamjomba", au "mkazahau". Kwa lugha ya baadhi ya makabila, na zaidi mjini Zanzibar anaitwa "mkwe" kwa sababu watoto wake unaweza kuoana nao.

Kwa baadhi ya makabila (Mf: Wabembe) mke wa mjomba anaitwa vilevile "mjomba" au "mjomba mwanamke". Hii ni kwa kuonesha tofauti kati ya shangazi (yaani dada yake baba) na mjomba (kaka yake mama). Wakati huohuo kwa upande wa shangazi, ikiwa ameolewa, mume wake huitwa "babu".

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjomba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.