Milima ya Alborz
(Elekezwa kutoka Alborz)
Alborz (kwa Kiajemi: البرز, inatoholewa pia: Alburz, Elburz au Elborz) ni safu ya milima kaskazini mwa Iran. Inaanza kwenye mipaka ya Azerbaijan na Armenia kaskazini magharibi mwa Iran na kuendelea upande wa mashariki ikifuata mwambao wa kusini wa Bahari ya Kaspi. Inaishia kaskazini mashariki mwa Iran karibu na mipaka ya Turkmenistan na Afghanistan.
Tehran, mji mkuu wa Iran iko miguuni pa milima ya Alborz.
Mlima Damavand ambao ni mlima mrefu zaidi katika Mashariki ya Kati, unapatikana katika Alborz, si mbali na Tehran.
Viungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Alborz Mountains, Photos from Iran, Livius.
- Maps, Photos and a List of peaks
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima ya Alborz kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |