Herufi za Kiarabu

(Elekezwa kutoka Alfabeti ya Kiarabu)

Herufi za Kiarabu ni maandishi maalumu ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa herufi za Kiarabu, hasa lugha za nchi zenye Waislamu wengi, ingawa herufi hizo zilibuniwa kabla ya dini hiyo kuenea. Kati ya lugha hizo kuna Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Pengine katika lugha hizo herufi kadhaa zinaongezwa au kupunguzwa, kulingana na lugha ilivyo.

"al-ABJaDiya al-arabiya" ni namna ya Kiarabu ya kusema "ABC ya Kiarabu"
(A-B-J-D ni herufi nne za kwanza za alfabeti ya Kiarabu).
Nchi zinazotumia herufi za Kiarabu:      kama mwandiko rasmi pekee      kama mwandiko mmojawapo.

Kihistoria hata Kiswahili na Kituruki ziliwahi kuandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa maumbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.

Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha silabi.

Herufi kuu

hariri
Umbo la herufi Jina Soma kama Alama za matamshi ya kimataifa
peke yake mwanzoni katikati mwishoni
أ, إ, ؤ, ئ
hamza ’ ‚ [ʔ]
alif ā [aː]
bāʾ b [b]
tāʾ t [t]
ṯāʾ th [θ]
ǧīm / j [ʤ]
ḥāʾ [ħ]
ḫāʾ / ẖ / kh [x]
dāl d [d]
ḏāl ḏ / dh [ð]
rāʾ r [r]
zāy z [z]
sīn s [s]
šīn š / sh [ʃ]
ṣād [sˁ]
ﺿ ḍād [dˁ]
ṭāʾ [tˁ]
ẓāʾ [ðˁ]
ʿayn ʿ / ‘ [ʕ]
ġayn ġ / gh [ɣ]
fāʾ f [f]
qāf q / ḳ [q]
kāf k [k]
lām l [l]
mīm m [m]
nūn n [n]
hāʾ h [h]
wāw w [w]
yāʾ y [jn]

Viungo vya nje

hariri