Ali bin Hamud wa Zanzibar
Ali bin Hamud (7 Juni 1884 - 20 Desemba 1918) alikuwa sultani wa Zanzibar kwa miaka tisa alitangazwa rasmi kuwa Sultani wa Zanzibar tarehe 20 Julai 1902, siku mbili kabla ya kifo cha baba yake aliyekuwa Sultani wa saba. Kulikuwa na utawala wa muda mfupi mpaka pale alipopata ridhaa ya wengi kuanza uongozi.
Ali bin Hamud wa Zanzibar | |
Sultani wa Zanzibar | |
Utawala wake | 20 Julai 1902 - 9 Desemba 1911 |
Mtangulizi wake | Hamoud bin Mohammed |
Mrithi wake | Khalifa bin Harub |
Tarehe ya kuzaliwa | 7 Juni 1884 |
Kifo chake | 20 Desemba 1918 (miaka 34)
Paris, France |
Alitumikia kiti hicho cha usultani kwa muda mfupi kutokana na maradhi. Tarehe 9 Desemba 1911 Ali alijiuzulu na kuacha kiti hicho kwa shemeji yake Khalifa bin Harub Al-Busaid.
Marejeo
hariri- The Politicization of Islam: Reconstructing Identity, State, Faith, and Community in the Late Ottoman State, ISBN 978-0-19-028576-0.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ali bin Hamud wa Zanzibar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |