Aliko Dangote
Aliko Dangote (alizaliwa 10 Aprili 1957) ni mfanyabiashara nchini Nigeria. Yeye ni mmiliki wa Dangote Group, ambayo ina shughuli katika Nigeria na nchi nyingine kadhaa za Afrika.
Aliko Dangote | |
Amezaliwa | 10 Aprili 1957 Kano, Nigeria |
---|---|
Kazi yake | Chairman & CEO, Dangote Group |
Wazazi | Alhaji Dangote |
Tovuti | dangote-group.com |
Msaidizi tajiri wa Rais mstaafu, Olusegun Obasanjo na chama tawala cha People's Democratic Party (PDP), Dangote huendesha biashara ya bidhaa ya Nigeria kupitia kampuni yake na kujuana na wanasiasa. Akiwa na mali ya karibu dola bilioni 2.5, alihesabiwa na Forbes kama mmoja wa watu wenye asili ya Afrika tajiri kabisa, nyuma ya Mohammed Al Amoudi (bilioni $ 9,0) na Oprah Winfrey (bilioni $ 2,7).[1]
Mnamo Novemba 2021, Sani Dangote, Makamu wa Rais (VP) wa Kundi la Dangote na mdogo wa Aliko Dangote, aliaga dunia.
Wasifu wa biashara
haririKundi la Dangote, awali biashara ndogo iliyoanzishwa mwaka 1977, sasa ni muungano wa makampuni mengi iliyo na thamani ya naira trilioni mingi na iliyo na oparesheni nchini Benin, Ghana, Nigeria na Togo. Biashara za Dangote ni pamoja na usindikaji wa chakula, utengenezaji saruji na kusafirisha mizigo. Kundi la Dangote linatawala soko la sukari nchini Nigeria, kwani yeye ndiye msambazaji mkubwa zaidi wa sukari nchini katika makampuni ya vinywaji laini, watengenezaji pombe na watengenezaji peremende. Kundi la Dangote limekua kutoka kwa biashara kampuni ya biashara hadi kuwa kundi kubwa zaidi la Viwanda nchini Nigeria, pamoja na kiwanda cha kusafishia sukari cha Dangote (kampuni iliyo na pesa zaidi katika Soko la Hisa la Nigeria, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 3 na usawa wa Aliko Dangote umefika bilioni $ 2), kiwanda kikubwa zaidi barani Afrika cha kutengeneza simiti: Obajana Cement, Kiwanda cha Unga cha Dangote miongoni mwa mengine.
Dangote alijihusisha pakubwa katika kufadhili kampeni ya Obasanjo ya kuchaguliwa upya katika uchaguzi wa mwaka 2003, ambapo yeye alichangia zaidi ya milioni N200 (milioni $ 2). Alichangia milioni N50 (milioni $ 0.5) Msikiti wa Taifa akitumia kikundi cha "Friends of Obasanjo na Atiku", akachangia milioni N200 (milioni $ 2) kwa hifadhi ya vitabu ya Rais. Zawadi hizo zenye utata kwa wanachama wa chama tawala cha People's Democratic Party zimechangia wasiwasi juu ya ufisadi licha ya kampeni za kupambana na rushwa zilizoongozwa na Obasanjo katika kipindi chake cha pili cha uongozi.
Tanbihi
haririMarejeo
hariri- Daudi S. Fick; Biashara katika Afrika: Masomo ya mafanikizi
Viungo vya nje
hariri- Mali ya Nigeria yakosa kufikia machinani
- Dangote Sukari, Kampuni tajiri zaidi Ilihifadhiwa 10 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Aliko Dangote: Mchezaji halisi wa wingi Ilihifadhiwa 10 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya kundi la Dangote Ilihifadhiwa 4 Aprili 2001 kwenye Wayback Machine.