Amber Reed
Amber Reed (alizaliwa 3 Aprili 1991) ni mchezaji wa raga cha Uingereza. Alishinda Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake 2014 kama mshiriki wa kikosi cha Uingereza na alichaguliwa kwa kikosi cha Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake ya 2017[1][2]. Kwa sasa anaichezea Bristol Bears.[3]
Jinsia | mwanamke |
---|---|
Nchi ya uraia | Ufalme wa Muungano |
Nchi anayoitumikia | Uingereza |
Jina halisi | Amber |
Jina la familia | Reed |
Tarehe ya kuzaliwa | 3 Aprili 1991 |
Mahali alipozaliwa | Bristol |
Relative | Andy Reed |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiingereza |
Kazi | rugby union player |
Alisoma | Collegiate School |
Mwanachama wa timu ya michezo | Bristol Bears, England women's national rugby union team |
Mchezo | rugby union |
Kazi
haririReed alichezea kwa mara ya kwanza katika timu ya raga ya Wanawake ya Uingereza mwaka 2012 dhidi ya Ufaransa, hapo awali aliichezea timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 20.
Mnamo 2014, alishinda Kombe la Dunia la Raga ya Wanawake akiwa na timu ya taifa ya Uingereza.
Alichaguliwa pia kwa timu ya Kombe la Dunia la Uingereza mnamo 2017, timu hiyo ilishindwa fainali na New Zealand.Alicheza pia katika mechi ya kwanza ya Wanawake wa Uingereza dhidi ya Barbarians huko Twickenham mnamo 2019, ambapo Uingereza ilishinda.Alichezea tena uingereza katika Mashindano ya Mataifa Sita ya Wanawake ya 2020.
Maisha ya awali
haririReed ni mpwa wa Andy Reed mchezaji wa awali wa timu ya taifa la Scotland. Akiwa kijana, aliichezea kriketi Gloucestershire na mpira wa magongo kwa Bristol. Alihudhuria Shule ya Colston na akaendelea kupata digrii ya Sayansi ya Mazoezi na Michezo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter. Alitajwa kuwa Mwanamichezo wa Vyuo Vikuu vya Uingereza vya Mwaka wa 2013.
Marejeo
hariri- ↑ "England announce squad for 2017 Women’s Rugby World Cup", RFU, 29 June 2017. Retrieved on 2022-05-14. (en) Archived from the original on 2017-10-04.
- ↑ Mockford, Sarah. "England name their squad for their Women's Rugby World Cup defence", Rugby World, 2017-06-29. (en-US)
- ↑ "Amber Reed". Bristol Bears (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-26.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amber Reed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |